Lugha Nyingine
Xi Jinping asema China itafungua zaidi mlango na kuendelea kujenga Jumuiya ya Binadamu yenye mustakabali wa pamoja
Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akizungumza na waandishi wa habari kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China Oktoba 23, 2022. Xi Jinping na viongozi wengine wapya waliochaguliwa wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 20 ya CPC, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi walikutana na waandishi wa habari jana Jumapili. (Xinhua/Li Xueren)
BEIJING – China itafungua mlango wake zaidi kwa Dunia, Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema Jumapili.
Pia siku hiyo, Xi ameeleza dhamira ya China ya kuendeleza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
"Tutakuwa imara katika kuimarisha mageuzi na kufungua mlango katika pande zote, na katika kutafuta maendeleo ya kiwango cha juu," Xi amesema alipokutana na waandishi wa habari kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing China, huku akieleza kuwa, China yenye ustawi itatoa fursa nyingi zaidi kwa Dunia.
“Kama ilivyo kwamba China haiwezi kujiendeleza kwa kutengwa na Dunia, pia Dunia inaihitaji China kwa maendeleo yake,” Xi amesema.
Amesema, kwa zaidi ya miaka 40 ya mageuzi na kufungua mlango bila kuchoka, China imefanya miujiza miwili ya ukuaji wa haraka wa uchumi na utulivu wa muda mrefu wa kijamii.
Uchumi wa China una uwezo mkubwa wa kustahimili uthabiti na umuhimu wake kwa Dunia, Xi amesema. "Misingi yake yenye nguvu haitabadilika, na itabaki kwenye mwelekeo mzuri kwa muda mrefu."
Kuhusu ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa baadaye, Xi amesema, China itashirikiana na watu wa nchi nyingine zote kutetea maadili ya pamoja ya binadamu ya amani, maendeleo, haki, usawa, demokrasia na uhuru ili kulinda amani ya kimataifa na kuhimiza maendeleo ya kimataifa, na kuendelea kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Huku akisisitiza kuwa Dunia inakabiliana na changamoto ambazo hazijawahi kushuhudiwa, Xi amesema CPC imekuwa ikitoa wito kwa watu wa Dunia kufahamu na kujenga siku nzuri za baadaye za binadamu.
"Nchi zote zinapofuata nia ya manufaa ya pamoja, tunaweza kuishi kwa maelewano, kushiriki katika ushirikiano kwa manufaa ya pande zote na kushikana mikono ili kuvumbua mustakabali mwema kwa Dunia," ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma