Maafisa Waandamizi wafafanua ripoti muhimu ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliomalizika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2022

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ikifanya mkutano na waandishi wa habari Tarehe 24 Oktoba 2022 ili kutambulisha na kufafanua ripoti muhimu ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliomalizika hivi punde. (Xinhua/Jin Liangkuai)

BEIJING - Ripoti ya Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliomalizika hivi punde, ni ilani ya kisiasa na mwongozo wa hatua za kufikia ushindi mpya juu ya ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya, afisa mwandamizi amesema Jumatatu.

Jiang Jinquan, Mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti wa Sera ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Beijing amesema ni uthibitisho wa hekima ya pamoja ya CPC na umma, iliyotokana na mchakato unaojumuisha demokrasia ya ndani ya chama na mchakato mzima wa demokrasia ya umma.

“Ripoti hiyo itakuwa na ushawishi mkubwa na muhimu juu ya sababu ya kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote na kuendeleza ustawi wa Taifa la China katika sekta zote, na itasaidia jumuiya ya kimataifa kuelewa vyema falsafa ya uongozi ya CPC, mtazamo wake wa usimamizi na uwezo wake wa kutawala” amesema.

Amesema kuwa, ripoti hiyo imeeleza namna CPC itakavyoboresha na kutekeleza Umarx, pia imeweka "ubora wa maendeleo" katika vipaumbele muhimu zaidi na inasisitiza maendeleo ya kiwango cha juu katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uchumi, jamii, utamaduni na ikolojia.

“Inathibitisha maendeleo ya kiwango cha juu ni kipaumbele cha juu cha kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa, na uthibitisho huo unaonyesha kwa nini ubora wa maendeleo ni muhimu kwa picha ya jumla na kwa muda mrefu” Mu Hong, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kamati ya kitaifa ya Mageuzi ya Kina na Naibu Mkuu wa Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Chen Yixin, Katibu Mkuu wa Kamati ya Siasa na Sheria ya Kamati Kuu ya CPC, ripoti hiyo ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC pia imeelezea umuhimu wa kusimamia utawala wa sheria, wazo la kuboresha mifumo ya chama na serikali kujisimamia kamili na kwa nidhamu kali na pia inahimiza Chama kizima kuzingatia kwamba kujisimamia kamili na kwa nidhamu kali ni juhudi isiyokoma na kwamba kujirekebisha ni safari isiyo na mwisho. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha