

Lugha Nyingine
Msomi wa Eritrea asema Chama cha CPC kina uwezo mkubwa wa utawala
Msomi kutoka nchini Eritrea Dr. Henok Neguse Negash amesema Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kina uwezo mkubwa wa utawala.
Dr. Henok amesema hayo alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), wakati Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China ukiendelea mjini Beijing.
Amesema kutokana na uongozi wa CPC, China imepata mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo jamii, uchumi, utamaduni, sayansi na teknolojia, na imekuwa nchi kubwa ya pili kiuchumi duniani. Kila mwaka, thamani ya biashara ya China inazidi bilioni moja, na imefanya juhudi kubwa za kuondoa umaskini. Pia amesema, China imepata maendeleo makubwa katika teknolojia, miji imestawi, huku uwekezaji katika elimu ukiongezeka. Anaona kuwa maendeleo na mafanikio hayo yanatokana na uongozi bora wa chama cha CPC, na juhudi za pamoja za serikali na wananchi wote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma