Uongozi wa CPC wapanga mikakati ya kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano wake Mkuu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 26, 2022

BEIJING - Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) siku ya Jumanne ilifanya mkutano ili kuweka mikakati na mipango ya kusoma, kueneza na kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliomalizika hivi karibuni.

Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ameongoza kikao hicho, ambacho pia kilijadili kanuni za kuimarisha na kulinda uongozi wa pamoja wa Kamati Kuu ya Chama, na kanuni za kina za utekelezaji wa uamuzi wa mambo mnane kuhusu mwenendo wa kazi.

“Kusoma, kueneza na kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC ni kazi ya msingi ya kisiasa kwa Chama na nchi kwa sasa na kwa muda ujao,” mkutano umesema.

Mkutano huo umeagiza kuelewa kwa kina umuhimu wa kuamua na kuthibitisha kwa nafasi kuu ya Komredi Xi Jinping katika Kamati Kuu ya Chama na katika Chama kwa ujumla na jukumu la kuongoza la Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalumu wa China kwa Zama Mpya.

Pia umesisitiza uelewa wa masuala makuu kuhusu Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalumu wa China kwa Zama Mpya, kuendana na muktadha wa China na mahitaji ya zama, na safari ya China kuelekea maendeleo ya kisasa.

Uelewa wa mipango ya kimkakati iliyowekwa na Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC kwa ajili ya kuijenga China kuwa nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote umesisitizwa katika mkutano huo.

Mkutano huo umesisitiza kuwa mipangilio na mahitaji yaliyowekwa na Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC yanafaa kutekelezwa katika nyanja zote za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Pia umesisitiza kujiandaa kiakili na kikazi kwa kila aina ya masuala magumu.

Kudumisha na kuimarisha uongozi wa pamoja wa Kamati Kuu ya CPC ni jukumu la wakati wote la kisiasa la Chama kizima, mkutano huo umesisitiza.

Umesisitiza kudumisha kiwango cha juu cha msimamo wa pamoja wa kifikra, kisiasa na kivitendo na Kamati Kuu ya CPC chini ya uongozi wa Komredi Xi Jinping.

Mkutano huo pia umesisitiza juhudi zinazoendelea katika kushughulikia matatizo ya taratibu kwa ajili ya taratibu na urasimu, na kudumisha uhusiano wa karibu na wananchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha