Xi Jinping asisitiza kusoma, kuelewa na kutekeleza malengo na majukumu yaliyotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa CPC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2022

BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Jumanne ya wiki hii amesisitiza kusoma, kuelewa na kutekeleza kikamilifu malengo na majukumu yaliyotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC ili kufanya juhudi katika kutafuta maendeleo mapya katika kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika mambo yote.

Xi ameyasema hayo alipokuwa akiongoza na kuhutubia semina elekezi ya kwanza ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 20 ya CPC.

Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi wametoa mawazo yao kuhusu kuelewa na kutekeleza misingi ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC. Walisema mkutano mkuu huo umetoa miongozo ya kimsingi kwa juhudi za CPC na nchi ya China katika safari mpya katika zama mpya, viongozi hao wameelezea nia yao ya kushikilia kithabiti nafasi kuu ya Xi kwenye Kamati Kuu ya Chama na katika Chama kwa ujumla, na pia kushikilia mamlaka na uongozi wa juu wa pamoja wa Kamati Kuu ya CPC na Xi akiwa katibu mkuu wake.

Katika hotuba yake kwenye semina elekezi hiyo, Xi amesema kuwa kusoma, kueneza na kutekeleza malengo na majukumu yaliyotolewa kwenye Mkutano Mkuu wa CPC itaendelea kuwa kazi kuu ya kisiasa kwa Chama kizima na nchi nzima.

Huku akisisitiza juhudi za kuelewa kwa kina mantiki ya kihistoria, kinadharia na ya kivitendo ya sera za kimsingi na mipangilio ya kimkakati iliyowekwa kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC kwa ajili ya Chama na nchi.

Ameagiza kuwepo kwa uelewa mpana wa maono ya Dunia na mbinu ya Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalumu wa China kwa Zama Mpya pamoja na misimamo, mitazamo na mbinu zake za kimsingi.

“Athari za kina na umuhimu wa mabadiliko makubwa yanayotokea katika muongo uliopita wa zama mpya unapaswa kueleweka kikamilifu,” Xi ameongeza.

Pia ametaka ufahamu kamili wa Umaalumu wa China na mahitaji muhimu ya maendeleo ya kisasa ya China na kanuni muhimu zinazopaswa kuzingatiwa kwa uthabiti, na mipango ya kimkakati iliyopitishwa katika Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

“Wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China wanapaswa kuongoza katika kushikilia mamlaka ya Kamati Kuu ya CPC na uongozi wake wa juu na wa pamoja”, Xi amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha