Wanafunzi wageni nchini China wataka kuimba nyimbo za kuwawezesha watu wa dunia waijue China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 01, 2022
Wanafunzi wageni nchini China wataka kuimba nyimbo za kuwawezesha watu wa dunia waijue China
Picha ikionesha wanabendi wakifanya mazoezi ya kuimba wimbo bwenini. (Picha/Li Yunhan)

“Hapo zamani ulichojua cha China ni Ukuta Mkuu, Kasri la Ufalme na Mto Changjiang, lakini sasa unachojua cha China ni uvumbuzi, reli ya mwendo kasi, 5G na chombo cha Tiangong kwenye anga ya juu.” Katika wimbo mpya wa “nikujulishe kuhusu China” uliotungwa na bendi ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, wanafunzi wageni wanaosoma nchini China wakiimba wimbo wameonyesha upendo wao kwa China.

Bendi ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ilianzishwa na wanafunzi wageni wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Usafiri wa Ndege cha Nanchang mwaka 2013 kwa njia ya kujitolea, katika bendi hiyo kuna wanafunzi kutoka nchi au maeneo ya India, Bangladesh, na Afrika Kusini. Hivi sasa, kwenye bendi hiyo kuna mwimbaji mkuu ambaye pia ni mcheza piano Mnyaga Daniel Rukiko kutoka Tanzania, mcheza bass Abel Jacob Chulu kutoka Zambia, mpiga ngoma Isaiah Nyasha Chikomo na mwimbaji mkuu Audrey Tanaka Murungweni kutoka Zimbabwe.

“Tumekusanyika kwa sababu ya kupenda muziki. Wanabendi wengi wa bendi yetu wanatoka nchi zilizoko kwenye “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, hali hiyo imeleta jina la bendi yetu.” Bw. Daniel alisema, wanapotunga wimbo wanaunganisha mitindo ya nyimbo za nchi zao pamoja na utamaduni wa China, ili kuimba nyimbo kwa kuonyesha dunia upendo wao kwa China.

“Tunatarajia watu wengi zaidi watasikiliza uimbaji wetu wa nyimbo , na kuwawezesha watu wengi zaidi wajue utamaduni wa China na maisha yetu halisi hapa China,”alisema Daniel. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha