

Lugha Nyingine
Bei za wanunuzi wa bidhaa nchini China zaimarika, huku bei za bidhaa za viwandani zikishuka
Watu wakinunua vitu kwenye supamaketi katika Mji wa Zaozhuang, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Oktoba 14, 2022. (Picha na Sun Zhongzhe/Xinhua)
BEIJING - Fahirisi ya bei ya wanunuzi bidhaa nchini China (CPI), kipimo kikuu cha mfumuko wa bei, ilipanda kwa asilimia 2.1 Mwezi Oktoba, ikipungua kutoka ukuaji wa asilimia 2.8 Mwezi Septemba, Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) imesema Jumatano.
Mtakwimu mkuu wa NBS Dong Lijuan amehusisha ufanisi huo thabiti wa CPI na mahitaji yanayopungua baada ya likizo ya Sikukuu ya Taifa ya China na msingi wa juu wa ulinganisho wa mwaka uliopita.
CPI ya msingi, ambayo haijumuishi bei ya chakula na nishati, ilipanda kwa asilimia 0.6 Mwezi Oktoba, bila kubadilika kutoka mwezi uliopita.
Bei za vyakula zilipanda kwa asilimia 7 mwaka hadi mwaka, zikipunguza asilimia 1.8 kutoka ile ya Mwezi Septemba, wakati bei zisizo za vyakula zilipata ongezeko la kila mwaka la asilimia 1.1, ikipunguza asilimia 0.4 kutoka mwezi uliopita.
“Bei za mboga mboga, matunda na bidhaa za majini zilibadili ongezeko la Septemba na kushuka kwa asilimia 4.5, asilimia 1.6 na asilimia 2.3, mwezi baada ya mwezi, mtawalia, huku bidhaa nyingi zikiingia sokoni na mahitaji kudhoofika,” Dong ameeleza.
Nyama ya nguruwe, nyama inayoliwa zaidi nchini China, ilishuhudia bei ikiongezeka kwa asilimia 51.8 mwezi Oktoba , ikipanuka kwa asilimia 15.8 zaidi ya mwezi uliopita. “Kupanda kwa bei ya nguruwe kulichangiwa zaidi na uhaba wa usambazaji, uimarishaji wa kimsimu wa mahitaji ya watumiaji, na ‘kusitasita kuuza’ sokoni, Dong amesema.
Kuweka bei za wanunuzi wa bidhaa katika uimara ni ajenda ya kipaumbele kwa serikali, kwani China imechukua hatua za kutolewa kwa makundi sita ya hifadhi kuu ya nguruwe kwenye soko. China pia itaimarisha ufuatiliaji wa soko na tahadhari ya mapema ya bei za mahitaji ya kila siku na kurahisisha usafirishaji wa mahitaji ya kila siku ili kuhakikisha ugavi wa kutosha na bei thabiti.
Takwimu hizo za Jumatano pia zinaonyesha fahirisi ya bei ya wazalishaji bidhaa wa China, ambayo hupima gharama za bidhaa kwenye lango la kiwanda, ilishuka kwa asilimia 1.3 mwaka hadi mwaka katika kipindi cha Mwezi Oktoba.
“Idadi hiyo imepungua kutoka kwa ongezeko la asilimia 0.9 la mwaka hadi mwaka lililorekodiwa Mwezi Septemba kutokana na ulinganifu wa juu katika kipindi kama hicho mwaka jana,” amesema Dong Lijuan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma