Rais Xi Jinping aongoza Maonyesho ya Uagizaji Bidhaa ya China kwenye Jukwaa la Kimataifa kwa kushiriki fursa za China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 11, 2022

SHANGHAI - Yakiingia katika awamu yake ya tano mwaka huu, Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji bidhaa ya China (CIIE) huko Shanghai yamekuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kimataifa, na "lango la dhahabu" la kuingia kwenye soko la China.

Maonyesho ya mwaka huu yameshirikisha nchi, kanda na mashirika ya kimataifa 145. Makampuni ya biashara kutoka nchi na maeneo 127 yameshiriki katika maonesho hayo.

Jumla ya makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 73.52 za Kimarekani ilifikiwa kwa ununuzi wa bidhaa na huduma wa mwaka mmoja kwenye maonyesho hayo ya tano ya CIIE, yaliyohitimishwa Alhamisi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.9 kuliko mwaka uliopita .

Picha hii iliyopigwa Tarehe 2 Novemba 2022 ikionyesha lango la Magharibi la Kituo cha Taifa cha Mikutano na Maonyesho cha Shanghai, ukumbi mkuu wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), huko Shanghai, nchini China. (Xinhua/Fang Zhe)

Likiwa ni wazo la Rais wa China Xi Jinping, CIIE ni maonyesho ya kwanza duniani ya uagizaji bidhaa yanayofanyika katika ngazi ya kitaifa.

Rais Xi yeye mwenyewe binafsi, amependekeza, ametuma na kuendeleza maonyesho hayo. Kwa miaka mitano mfululizo, hotuba na kauli za Rais Xi zimeashiria kwa Dunia kuwa, China itazifungulia mlango zaidi nchi za duniani.

Ahadi iliyotimizwa

Katika hotuba yake kuu kwenye hafla ya ufunguzi wa maonesho ya kwanza ya CIIE Mwaka 2018, Xi alisema maonyesho hayo ni "uamuzi muhimu uliofanywa na China kutekeleza awamu mpya ya kufungua mlango kwenye kiwango cha juu, na ni mpango mkuu wa China wa kupanua wigo wa soko kwa Dunia nzima."

Jukumu kuu la Xi lilisaidia kuongoza maonesho ya kwanza ya CIIE kwa mafanikio makubwa. Zaidi ya makampuni 3,600 ya kimataifa yalishiriki katika maonyesho ya kwanza, na kufikia makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 57.8 za Kimarekani

Katika miaka mitano iliyopita, Xi, kupitia kila maonyesho, amekuwa akisisitiza ahadi ya China ya kufungua mlango. CIIE imeshuhudia Rais Xi akitangaza mfululizo wa hatua madhubuti za kuhimiza uchumi na biashara ya Dunia na ya nchini China.

Watu wakitembelea eneo la maonyesho ya Teknolojia za Akili Bandia na Teknolojia ya Habari la Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) huko Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 5, 2022. (Xinhua/Fang Zhe)

Bidhaa za Umma

Takwimu zinaonyesha kuwa, kuanzia Mwaka 2018 hadi 2021, washiriki katika awamu nne za maonyesho ya CIIE walileta zaidi ya bidhaa, teknolojia na huduma mpya 1,500, na mauzo ya majaribio yanazidi dola za Kimarekani bilioni 270.

"Tunahitaji kuhimiza maendeleo kwa kufungua mlango na kuimarisha mabadilishano na ushirikiano kati yetu. Tunahitaji 'kushikana mikono' badala ya 'kuachiana' mikono ya kila mmoja wetu. Tunapaswa 'kubomoa kuta,' siyo kusimamisha kuta.' Tunahitaji kusimama kidete dhidi ya kujifungia kiuchumi na misimamo ya upande mmoja," Xi alisema katika maonesho ya pili ya CIIE Mwaka 2019.

Picha hii iliyopigwa Novemba 2, 2022 ikionyesha gari la kifahari la Hummer EV aina ya SUV la General Motors Co. (GM) kwenye banda la Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) huko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)

Mustakabbali wa Pamoja

Akihutubia awamu ya kwanza ya maonesho ya CIIE, Xi alisema, maonesho hayo yatafanyika kila mwaka na "yatahusisha ufanisi mzuri, matokeo mazuri na mafanikio endelevu katika miaka ijayo."

"Mafanikio ya CIIE kwa mwaka wa tano mfululizo yanaonyesha uthabiti mkubwa wa uchumi wa China na ukubwa wake wa soko." anasema Hann Pang, Mkuu wa Kampuni ya Thermo Fisher, Tawi la China. 

Hafla ya kutia saini kwa washiriki wa Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) ikifanyika huko Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 6, 2022. (Xinhua/Fang Zhe)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha