Wanaanga wa China kwenye chombo cha Shenzhou-14 waingia kwenye chombo cha mizigo cha Tianzhou-5

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 14, 2022

Picha hii ya skrini iliyopigwa kwenye Kituo cha Udhibiti wa Safari ya Anga ya Juu cha Beijing Novemba 12, 2022 ikionyesha mwonekano wa ndani wa moduli ya Tianhe baada ya chombo cha anga ya juu cha China cha Tianzhou-5 kufanya michakato ya kiotomatiki na kutia nanga pamoja na mchanganyiko wa kituo cha anga ya juu cha China cha Tiangong. (Picha na Sun Fengxiao/Xinhua)

BEIJING – Wanaanga wa China kwenye chombo cha Shenzhou-14 wameingia kwenye chombo cha mizigo cha Tianzhou-5 siku ya Jumapili, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA).

“Wamefungua mlango wa hatch ya Tianzhou-5 saa 8:18 mchana. (Saa za Beijing) na kuingia kwenye chombo cha anga ya juu saa 9:03 alasiri (Saa za Beijing) kufuatia kazi ya maandalizi,” imesema CMSA.

Wanaanga hao kwenye chombo cha Shenzhou-14 watafanya uhamisho wa mizigo na kazi nyingine zinazohusiana kama ilivyopangwa.

China ilirusha kwenye anga ya juu chombo cha Tianzhou-5 siku ya Jumamosi ili kupeleka vifaa kwa ajili ya kituo cha anga ya juu cha nchi hiyo, ambacho ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwaka huu.

Roketi ya Long March-7 Y6, iliyokuwa imebeba chombo cha Tianzhou-5, iliruka Saa 4:03 asubuhi (Saa za Beijing) siku ya Jumamosi kutoka Eneo la Urushaji wa Vyombo kwenye Anga ya Juu la Wenchang katika Mkoa wa kisiwa wa Hainan, Kusini mwa China.

Takriban saa mbili baadaye, Tianzhou-5 ilifanya michakato ya kiotomatiki na kutia nanga kwenye nyuma ya moduli ya msingi ya kituo cha anga ya juu cha China, Tianhe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha