Rais Xi Jinping atoa wito wa kujenga uhusiano kati ya China na Japan kuendana na zama mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2022

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida mjini Bangkok, Thailand, Novemba 17, 2022. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping amesema China iko tayari kushirikiana na Japan ili kuweka uhusiano wa pande hizo mbili kwenye njia sahihi kutoka kwenye ngazi ya kimkakati, na kujenga uhusiano kati ya China na Japan uendane na zama mpya.

Rais Xi ameyasema hayo alipokutana na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Viongozi wa nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC).

Akieleza kuwa China na Japan kwa pamoja mwaka huu zimefikisha miaka 50 tangu uhusiano wa kidiplomasia uliporejeshwa katika hali ya kawaida, Xi amesema katika miongo mitano iliyopita, pande hizo mbili zimesaini nyaraka nne za kisiasa za China na Japan, kufikia maelewano kadhaa muhimu ya pamoja, na kufurahia mabadilishano na ushirikiano wenye manufaa katika maeneo mbalimbali.

“Haya yote yameleta matunda muhimu kwa watu wa pande mbili na kuchangia amani ya kikanda, maendeleo na ustawi. China na Japan zikiwa majirani wa karibu na nchi muhimu barani Asia na duniani zina maslahi mengi ya pamoja na nafasi ya kutosha ya ushirikiano. Umuhimu wa uhusiano kati ya China na Japan haujabadilika na hautabadilika,” amesema Rais Xi.

Rais Xi amesisitiza kuwa, pande hizo mbili zinahitaji kutendeana kwa dhati na kushirikishana kwa uaminifu, kufuata kanuni zilizowekwa kwenye nyaraka nne za kisiasa za China na Japan, kujumuisha na kukumbuka mafunzo ya historia, zinahitaji kutazama maendeleo ya kila mmoja wao katika lengo na njia yenye busara, na kutafsiri katika sera makubaliano ya kisiasa kwamba nchi hizo mbili zinapaswa "kuwa wenzi wa ushirikiano, kila upande sio tishio dhidi ya upande mwingine ."

“Masuala makuu ya msimamo kama vile historia na Taiwan yana msingi wa kisiasa na kuaminiana kimsingi katika uhusiano wa China na Japan, na kwa hivyo lazima yashughulikiwe kwa nia njema na ipasavyo. China haiingilii mambo ya ndani ya nchi nyingine, wala haikubali kisingizio chochote cha mtu kuingilia mambo yake ya ndani,” amesema Rais Xi.

Rais Xi amesema, kuhusu masuala yanayohusu migogoro ya bahari na maeneo mengineyo, ni muhimu kufuata kanuni na maelewano ya pamoja ambayo yamefikiwa, na kuonyesha hekima ya kisiasa na uwajibikaji wa kudhibiti ipasavyo tofauti.

Amesema, uchumi wa nchi hizo mbili ukitegemeana kwa kiwango kikubwa, nchi hizo mbili zinahitaji kuongeza mazungumzo na ushirikiano katika nyanja kama vile uchumi wa kidijitali, maendeleo ya kijani, sekta za mambo ya fedha, huduma za afya na huduma za wazee na kuweka minyororo ya viwanda na ugavi kuwa thabiti na isiyozuiliwa.

Rais Xi pia amesisitiza haja ya China na Japan kukataa migogoro na mapambano, kufanya ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kuhimiza mchakato wa mafungamano ya kikanda, kushirikiana pamoja kwa ajili ya kuendeleza vizuri na kujenga vizuri Bara la Asia , na kukabiliana na changamoto za kimataifa.

Kwa upande wake, Kishida amekumbuka mawasiliano kwa njia ya simu na Rais Xi ya Oktoba mwaka jana, ambapo walikubaliana kujenga uhusiano wa Japan na China ili uendane na zama mpya, alisema, hivi sasa mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali yanarejea hatua kwa hatua.

Huku akisema juu ya suala la Taiwan, hakuna mabadiliko yoyote katika ahadi zilizotolewa na Japan, amesisitiza kuwa kama majirani wa karibu, Japan na China, kila upande hauna tishio kwa upande mwingine. Pande zote mbili zinahitaji na zinapaswa kuishi pamoja kwa amani.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida mjini Bangkok, Thailand, Novemba 17, 2022. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha