Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asema China imejitolea kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja
Nembo ya Mkutano wa Viongozi wa nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Nchi za Asia na Pasifiki wa Mwaka 2022 (APEC 2022) ikionekana katika picha mtaani Bangkok, Thailand, Novemba 16, 2022. (Xinhua/Wang Teng)
BANGKOK - Rais wa China Xi Jinping Alhamisi amesisitiza kwamba China imejitolea kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja, na itafanya juhudi zaidi za kuimarisha utulivu na ustawi wa eneo la Asia-Pasifiki.
Rais Xi ameyasema hayo katika hotuba yake ya maandishi, yenye kichwa kisemacho "Kushikilia nia ya awali, Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo, na Kufungua Ukurasa Mpya wa Ushirikiano wa Asia-Pasifiki”, kwenye Mkutano wa Viongozi wa nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC).
Amesema, Dunia kwa mara nyingine imefikia njia panda. Inaelekea wapi? Asia-Pasifiki inapaswa kufanya nini? Maswali haya yanahitaji majibu ya haraka.
“Katika miongo kadhaa iliyopita, wanachama wa eneo hili wametoka mbali katika kutafuta maendeleo ya kiuchumi. Ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki umeingiza msukumo mkubwa katika maendeleo ya eneo hili na kuboresha sana ustawi wa watu wake. Wanachama wa eneo hili wanapaswa kutumia uzoefu muhimu wa zamani na kubaki thabiti katika kufuata malengo yao ya maendeleo” Rais Xi amesema.
Amesisitiza haja ya kufuata njia ya maendeleo ya amani, kwa sababu Asia-Pasifiki iliachiliwa kutoka kwenye kivuli cha Vita Baridi, eneo hili, na hasa uchumi wake mdogo na wa kati, umeweza kuanza safari ya haraka kuelekea maendeleo ya kisasa na kutengeneza muujiza wa Asia-Pasifiki.
“Asia-Pasifiki siyo ua wa mtu yeyote na haifai kuwa uwanja wa mashindano ya nchi zenye nguvu kubwa. Hakuna jaribio la kufanya vita baridi mpya litakaloruhusiwa na watu au na nyakati,” amesema Rais Xi.
Amesisitiza haja ya kufuata njia ya kufungua mlango na kufanya ushirikiano na pande nyingi. Amesema, katika miongo kadhaa iliyopita, APEC, ikifuata njia hiyo ya kikanda na kushikilia kanuni za kuwepo kwa hali mbalimbali tofauti na kutobaguana, imekuwa na usanifu wa ushirikiano wa kikanda unaojumuisha na wa kunufaishana.
Rais Xi ametoa mapendekezo sita kama ifuatavyo;
Kwanza, kuimarisha msingi wa maendeleo ya amani. Amesema, ni muhimu kufuata nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, kufuata maono ya usalama wa pamoja, wa pande zote, wenye ushirikiano na endelevu, kukataa kwa pamoja mawazo ya Vita Baridi na makabiliano ya kambi, na kujenga muundo wa usalama wa Asia-Pasifiki.
Pili, kufuata mtazamo wa maendeleo ambayo watu ni msingi wake . Amesema, mengi zaidi yanapaswa kufanywa ili kuhakikisha ustawi wa watu kupitia maendeleo ya kiuchumi na kuendeleza mazingira jumuishi ya maendeleo.
Tatu, kufuata kufungua mlango kwa kiwango cha juu ambapo amesema ni muhimu kuendeleza ujenzi wa Eneo la Biashara Huria la Asia-Pasifiki, kushiriki kikamilifu na kwa pande zote katika mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani (WTO).
Nne, kujitahidi kwa muunganisho wa kiwango cha juu, tano, kujenga minyororo ya viwanda na ugavi imara na isiyozuiliwa na mwisho, kuhimiza maendeleo na uboreshaji wa uchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma