Tamaa kwa gesi asilia ya Afrika yaleta wasiwasi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2022

Wataalamu wasema ufuatiliaji wa nchi za Magharibi kwa mafuta ya Afrika watishia lengo la tabianchi

Katika mazungumzo kuhusu tabianchi nchini Misri, nchi za Magharibi zinazofuatilia akiba ya gesi asilia ya Afrika zililaumiwa vikali zaidi.

Kwa kukabiliwa na upungufu wa nishati uliosababishwa na mgogoro kati ya Russia na Ukraine, nchi nyingi za Magharibi zinatarajia Afrika iwe chanzo mbadala cha nishati. Lakini walinda mazingira ya asili wametoa maonyo, kwa sababu kumbukumbu za vitendo vya unyonyaji vya nchi hizo katika Afrika na sehemu nyingine duniani vimeongeza wasiwasi wao.

Joab Okanda, mshauri wa Shirika la Msaada wa Kikristo, ambalo ni shirika lisilo la kiserikali la Kenya alisema, hakuna sehemu nyingine yoyote duniani inayoathiriwa zaidi na matumizi ya nishati ya visukuku kuliko Afrika. Kwa hivyo bara la Afrika linatakiwa kuonyesha njia tofauti ya maendeleo kwa dunia.

“Makampuni ya nishati ya visukuku yanaonesha tamaa zao, na yanapanga kuhuisha nishati ya visukuku katika nchi 48 kati ya nchi 55 zote barani Afrika,” alisema Okanda.

Hali halisi “inayokasirisha”

“Inatukasirisha kuwa, asilimia 89 ya miundombinu ya gesi asilia ya kimiminika iliyotengenezwa barani Afrika itauzwa kwa Ulaya, ili kuwasaidia kujitoa kutoka kwenye tegemezi kwa gesi asilia ya Russia.”

Maelezo hayo yanatokana na ripoti ya “Nani anatoa mtaji kwa upanuzi wa nishati ya visukuku barani Afrika”, ambayo inaonesha kuwa, Marekani inaongoza katika ufadhili wa utafiti wa nishati ya visukuku barani Afrika katika mambo ya fedha na utaratibu.

Wanakampeni, watafiti na watu wa kundi la uteteaji walisema kwenye mkutano wa COP27 kuwa, uuzaji wa gesi asilia kwa nchi za nje huenda utaleta faida kwa muda mfupi, lakini utaongeza msukosuko wa tabianchi, na kufanya hali ya nchi za Afrika izidi kuwa mbaya katika muda mrefu wa siku za baadaye.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha