Mfumuko wa bei wa Marekani wasababisha bei za bata mzinga zapandishwe juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2022

Picha na Ma Hongliang(Tovuti ya Gazeti la Umma)

Kituo cha biashara cha Tovuti ya CNN kilisema Tarehe 16 kuwa ripoti mpya iliyotolewa na Shirikisho la Idara ya Kilimo la Marekani ikionesha kuwa kutokana na athari ya mfumuko wa bei, bei za chakula cha jioni cha Sikukuu ya Shukrani zitapandishwa juu kwa 20% kuliko zile za mwaka jana. Ripoti hiyo pia ilionesha kuwa wastani wa bei ya bata mzinga wenye uzito wa pauni 16 mwaka huu ni dola za kimarekani 28.96, ambayo imepandishwa kwa 21% ikilinganishwa ile ya Mwaka 2021.

Uchunguzi wa maoni ya watu uliotolewa na Gazeti ya The Times katikati ya mwezi Oktoba ulionesha kuwa mfumuko wa bei ni tatizo kubwa zaidi linaloikabili Marekani sasa. Takwimu za Idara ya Takwimu ya Wafanyakazi ya Marekani zinaonesha kuwa hivi majuzi, bei za matumizi za wakazi wa Marekani zimefika kiwango cha juu zaidi katika miaka ya 40 iliyopita. Mfumuko wa bei na bei za bidhaa zinazopandishwa kwa kasi zinawafanya watu wa Marekani wabane matumizi yao na kuongezwa mzigo zaidi wa maisha.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha