Kufungua mlango kwa upana zaidi kwa China kwaleta uhai kwa maendeleo ya kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2022

Mtembeleaji wa maonyesho akitazama gari kwenye banda la Toyota kwenye Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji bidhaa ya China (CIIE) huko Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 6, 2022. (Xinhua/Li Jing)

BEIJING - China imekuwa ikizungumzia kufungua mlango kwenye kiwango cha juu, na hatua madhubuti ambazo zitanufaisha uchumi duniani.

China imesisitiza tena Ijumaa ya mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba itaendeleza ajenda pana ya kufungua mlango katika sekta nyingi zaidi na kwa kina zaidi, kufuata safari ya maendeleo ya kisasa ya China, kuweka mifumo mipya kwa ajili ya uchumi ulio wa kufungua mlango kwenye kiwango cha juu, na kuendelea kushirikisha fursa za maendeleo ya China kwa Dunia.

Katika moja ya juhudi zake za hivi majuzi kufikia lengo hilo, China imefungua sekta zaidi kwa uwekezaji wa kigeni, na orodha yake mpya ya tasnia ambazo uwekezaji wa kigeni utahamasishwa. Marekebisho hayo, yenye vitu vipya 239 vilivyoongezwa na 167 vilivyopo kurekebishwa, yanaweka mkazo maalum katika sekta ya viwanda na huduma za wazalishaji.

Katika kufungua soko la fedha, China pia imeruhusu wawekezaji wa taasisi za ng'ambo wanaostahiki kuwekeza moja kwa moja au kupitia kuunganishwa katika soko la dhamana la kubadilishana fedha kuanzia Juni 30, mwaka huu.

Ikiungwa mkono na juhudi hizi, China imedumisha mvuto wake mkubwa kwa biashara za kigeni licha ya hisia mbaya za uwekezaji kote duniani. Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) katika China Bara, matumizi yake halisi yalipanda kwa asilimia 17.4 na kufikia dola za Kimarekani bilioni 168.34 katika miezi 10 ya kwanza mwaka huu, takwimu rasmi zinaonyesha.

Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), yaliyofanyika kuanzia Novemba 5 hadi Novemba 10, yalishuhudia jumla ya makubaliano ya kibiashara ya muda yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 73.5. Makubaliano hayo yamefikiwa kwa ununuzi wa mwaka mmoja wa bidhaa na huduma. Kiasi hicho kiliongezeka kwa asilimia 3.9 kuliko kile cha mwaka jana.

Maonyesho ya Sita ya China na Asia Kusini, yaliyofunguliwa Jumamosi huko Kunming, mji mkuu wa mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China, ni jukwaa lingine la China kushirikiana na nchi mbalimbali ili kujenga vichocheo zaidi vya ukuaji wa ushirikiano, kuendeleza maendeleo ya kiwango cha juu ya Ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, ili kujenga mustakabali mwema na mzuri zaidi pamoja.

Biashara ya nje ya China katika bidhaa na nchi na kanda zinazoshiriki katika Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja ilirekodi ukuaji, na mauzo ya nje na uagizaji bidhaa viliongezeka kwa zaidi ya asilimia 20, takwimu rasmi zinaonyesha.

Ripoti ya Benki ya Dunia imekadiria kuwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ifikapo Mwaka 2030, linaweza kusaidia kuwaondoa watu milioni 7.6 kutoka katika umaskini uliokithiri na watu milioni 32 kutoka katika umaskini wa wastani duniani kote. Pia litasaidia kuongeza mapato ya dunia kwa asilimia 0.7.

"China inayofungua mlango zaidi italeta maendeleo makubwa zaidi na ustawi wake binafsi na kwa Dunia," Cui Fan, profesa katika Chuo Kikuu cha Biashara ya Kimataifa na Uchumi cha China amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha