Ziara ya Rais Xi Jinping nje ya nchi yaonyesha dhamira ya China katika kuchangia ukuaji uchumi na uongozi wa kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2022

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amerejea China Jumamosi jioni kutoka kwenye ziara yake ya siku sita, ambapo alihudhuria Mkutano wa 17 wa Kundi la 20 (G20) na Mkutano wa 29 wa Viongozi wa nchi za Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC), na kufanya ziara nchini Thailand.

“Baada ya kukamilika kwa mafanikio kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mambo ya diplomasia ya nchi kubwa yameanza safari mpya,” Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China amesema.

Katika ziara yake hiyo ya siku sita, Xi alishiriki katika shughuli zaidi ya 30, ambazo zimetoa sauti kubwa kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya kimataifa na uongozi wa kimataifa, kuonyesha jukumu la China kama nchi kubwa yenye busara, ujasiri na kuwajibika, amesema Wang.

“Akihutubia mikutano ya pande nyingi na kuzungumza na viongozi wa nchi nyingine, Xi alieleza juu ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, maendeleo ya kisasa ya China, ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote kati ya China na Dunia nzima, na kuhimiza matarajio mazuri ya maendeleo ya China yenye kiwango cha juu na kufungua mlango kwenye kiwango cha juu, akituma ujumbe kwamba China itaendeleza maendeleo kwa amani na kuimarisha kufungua mlango na ushirikiano na nchi nyingine.” Wang amesema.

Katika mkutano wa G20, Xi alitoa wito kwa nchi zote kuwa na uelewa juu ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kutetea amani, maendeleo na ushirikiano wa kunufaishana, ili kuondoa migawanyiko kwa kuweka umoja, mapambano kwa kuweka ushirikiano na kutengana kwa kuweka ujumuishaji, na kufanya maendeleo ya kimataifa kuwa jumuishi zaidi na yenye manufaa kwa wote na yenye kustahimili zaidi.

Wang amesema, Rais wa China alipendekeza kujenga ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kufufua uchumi na Ushirikiano wa Kimataifa juu ya Usalama wa Chakula Duniani, na kuunga mkono Umoja wa Afrika (AU) kujiunga na G20, akionyesha kuwa Rais Xi amekuwa akizijali nchi zinazoendelea na kuendelea kujitolea kwa mawazo hayo.

Kwenye mkutano wa viongozi wa APEC Wang amesema kuwa Xi alifanya majumuisho kuhusu uzoefu uliofanikiwa na mafunzo katika ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki, huku akisisitiza kwamba Asia-Pasifiki si ua wa mtu na haipaswi kuwa uwanja wa nchi kubwa kugombea madaraka. Rais wa China alisema hakuna jaribio la kuanzisha Vita Baridi vipya litakaloruhusiwa na watu au na nyakati.

Wang amesema Xi alitoa wito wa kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja iliyo ya amani, utulivu, safi na uzuri, eneo ambalo nchi zote na watu wote wako tayari kusaidiana na huleta ustawi kwa wote.

Wang amesema, Xi alitangaza kuwa China inafikiria kufanya Kongamano la Tatu la Ukanda Mmoja na Njia Njia moja kwa Ushirikiano wa Kimataifa mwaka ujao ili kutoa msukumo mpya kwa maendeleo na ustawi wa Asia-Pasifiki na Dunia.

Xi pia alifanya mkutano wa ana kwa ana na Rais wa Marekani Joe Biden mjini Bali, ambapo walikuwa na mazungumzo ya wazi na ya kina kuhusu masuala muhimu ya uhusiano kati ya China na Marekani na yanayohusu amani na maendeleo duniani.

Xi pia alifanya mazungumzo na viongozi wa nchi mbalimbali wa duniani na kuzungumzia masuala yahusuyo uhusiano wa pande mbili mbili na yale ya kimataifa ikiwemo vita vya Ukraine, msukosuko wa nishati, usalama wa chakula, maendeleo ya kiuchumi na mabadiliko ya tabianchi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha