Mwanafunzi wa Malawi avumbua Glavu ya kusaidia mawasiliano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 22, 2022

Madalitso Mnduwira akionesha glavu ya sauti aliyoivumbua huko Blantyre, Malawi, Novemba 10, 2022. (Picha ilipigwa na Joseph Mizere/Xinhua)

Kama usemi unavyosema, “mahitaji huleta uvumbuzi”. Katika Chuo Kikuu cha Biashara na Sayansi ya Matumizi cha Malawi, mwanafunzi mmoja aliyeshindwa kuwasiliana vizuri na rafiki yake mwenye tatizo la kuongea, hali hii ilimfanya afikirie namna ya kusaidia mawasiliano hayo.

Madalitso Mnduwira, mwanafunzi huyu mwenye umri wa miaka 21 mwishowe alivumbua aina ya glavu, ambayo ukivaa glavu hiyo na kutumia lugha ya ishara ya mikono, glavu hiyo itatafsiri ishara yako na kutoa sauti ya Kiingereza au ya lugha nyingine za Kienyeji.

Mnduwira anasoma somo la TEHAMA chuoni. Katika mahojiano ya hivi karibuni na shirika la habari la China Xinhua, alimwambia mwandishi wa habari kuwa, kwa kupitia uvumbuzi huo, anatumai watu wenye ulemavu wanaohitaji kutumia lugha ya ishara wanaweza kuwasiliana na wengine kwa ufanisi.

Alifafanua kuwa, “Glavu ya sauti inatengenezwa kwa nyenzo za gharama ya chini, ambazo zinazalishwa katika sehemu alipoishi. Glavu ya aina hiyo itasaidia kuondoa pengo la mawasiliano kati ya watu wenye tatizo la usikivu na watu wengine.”

Kamati ya walemavu ya Malawi (MACOHA) pia imeonesha ufuatiliaji wake wa mawasiliano kwa kupitia “glavu ya sauti”.

Madalitso Mnduwira akionesha glavu ya sauti aliyoivumbua huko Blantyre, Malawi, Novemba 10, 2022. (Picha ilipigwa na Joseph Mizere/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha