Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa Mkutano wa 16 wa Taasisi ya Sayansi ya Nchi Zinazoendelea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 22, 2022

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatatu ametuma barua ya pongezi kwa Mkutano wa 16 wa Taasisi ya Sayansi ya Nchi Zinazoendelea na Mkutano wa 30 wa Wanataaluma.

Katika barua hiyo, Rais Xi amesema China inatilia maanani sana maendeleo ya sayansi ya kimsingi na iko tayari kushirikiana na nchi mbalimbali duniani, zikiwemo nchi zinazoendelea, ili kuongeza uwazi, kuaminiana na ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia za kimataifa, na kuwanufaisha watu wa nchi zote kupitia maendeleo yenye ustawi ya sayansi.

“China iko tayari kushirikiana na nchi zote kuchangia katika kuendeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, kutekeleza Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja,” Xi amesema.

Mikutano hiyo ilifunguliwa Jumatatu iliyopita huko Hangzhou mkoani Zhejiang, ambayo iliandaaliwa na Taasisi ya Sayansi ya nchi zinazoendelea na kuendeshwa na Chuo Kikuu cha Zhejiang cha China, na pia inaungwa mkono na Shirika la Sayansi na Teknolojia la China na Taasisi Kuu ya Sayansi ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha