Kongamano la ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika katika sekta ya utalii lafanyika kwa njia ya video

(CRI Online) Novemba 23, 2022

(Picha inatoka CRI.)

Kongamano la ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika katika sekta ya utalii lililoandaliwa na wizara ya utamaduni na utalii na Taasisi ya Utafiti wa Utalii ya China limefanyika kwa njia ya video. Wajumbe zaidi ya 30 kutoka mamlaka za utalii, taasisi za utafiti na kampuni za utalii za nchi 6 (China, Benin, Cameroon, Gabon, Côte d'Ivoire na Senegal) wameshiriki kwenye kongamano hilo.

Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Utalii ya China Bw. Dai Bin alipohutubia kongamano hilo alisema nchi na maeneo yaliyopo kwenye "Ukanda Mmoja, Njia Moja" zikiwemo nchi za Afrika, zimekuwa chanzo cha watalii kinachokua kwa kasi katika soko la utalii la China. Amependekeza China na nchi za Afrika ziimarishe ushirikiano katika utafiti wa sera ya utalii, masoko, elimu na mafunzo, huduma za mapokezi n.k. na kuweka sera zinazorahisisha usafiri na kuboresha huduma ya mapokezi ya kitalii.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Burudani ya Senegal Bw. Mamadou Bassirou Ndiaye, amesema Senegal inapendelea kuimarisha ushirikiano na China katika sekta ya utalii na kuvutia watalii wengi zaidi wa China kuitembelea Senegal. Na pia kwa niaba ya nchi za Afrika zinazoshiriki kwenye kongamano hilo, amesema zitashirikiana na China kuendelea kuhimiza uhusiano kati yao na China kwa kina chini ya mwongozo wa "Azimio la Dakar la Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC". 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha