Kikundi cha madaktari wa China chatoa huduma za matibabu bila malipo Zanzibar

(CRI Online) Novemba 25, 2022

Kikundi cha 32 cha madaktari wa China tarehe 17 kilitoa huduma za matibabu bila malipo katika kituo cha afya cha Fuoni, Zanzibar.

Shughuli hiyo ni kwa ajili ya kuwapatia watu wa Zanzibar huduma ya matibabu na upimaji wa afya bila malipo kwa magonjwa mbalimbali. Madaktari hao wa China waliwatibu wagonjwa zaidi ya 150 ndani ya saa nne, na kuwaelekeza wagonjwa zaidi ya 20 wapate matibabu kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Mkurugenzi wa kituo cha afya cha Fuoni alishukuru Kikundi cha madaktari wa China katika kutoa msaada wa kimatibabu unaowanufaisha watu wa huko. Mkuu wa kikundi cha 32 cha madaktari wa China huko Zanzibar Zhao Xiaojun, alisema kikundi chake kitaendelea kuwapatia watu wa huko huduma za matibabu zenye ubora.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha