Wanariadha wa Kenya huenda wakafungiwa kutokana na kesi za matumizi ya dawa za kusisimua misuli

(CRI Online) Novemba 25, 2022

Serikali ya Kenya inafanya juhudi za mwisho kukwepa uwezekano wa wanariadha wake kufungiwa kimataifa kutokana na kuongezeka kwa kesi za matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Wajumbe kutoka Mamlaka ya Kimataifa ya Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli (WADA), Kitengo cha Uadilifu cha Riadha (AIU) na Shirika la Kimataifa la Riadha wanatarajiwa kukutana mjini Monte Carlo, Monaco leo ijumaa kujadili hali ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli kwa wanariadha duniani, huku hali mbaya ya matumizi ya dawa hizo kwa wanariadha kutoka Kenya ikipewa kipaumbele.

Jana Alhamis, Waziri wa Michezo wa Kenya Ababu Namwamba alithibitisha kuwa serikali inachukua hatua kali kulinda na kudumisha uaminifu wa wanariadha na michezo mingine kwa ujumla.

Katika miaka mitano iliyopita, Kenya imeorodheshwa katika Ngazi A, kama nchi yenye kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha