UNECA yazitaka nchi za Afrika kuimarisha biashara ya ndani kukabiliana na mishtuko kutoka nje

(CRI Online) Novemba 25, 2022

Kaimu Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Uchumi barani Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Antonio Pedro amesisitiza haja ya nchi za Afrika kuboresha biashara ya ndani ili kukabiliana na mishtuko kutoka nje.

Akizungumza katika Jukwaa la Ngazi ya Juu la Umoja wa Afrika lililofanyika mjini Niamey, Niger, Pedro amesema Afrika inayofanya biashara kubwa ya ndani katika bidhaa za aina mbalimbali ni chaguo bora zaidi katika kujenga Afrika yenye uhimillivu wa kiuchumi inayoweza kuvumilia changamoto zinazotoka nje ya bara hilo.

Amesema bara la Afrika limepata changamoto kubwa kuliko maeneo mengine kutokana na janga la COVID-19 na athari za mgogoro nchini Ukraine, na hii inatokana kwa kiasi kikubwa na utegemezi wake wa kuagiza bidhaa nje. Pia amesisitiza kuwa mageuzi endelevu ya kiuchumi ya Afrika yanahitaji ukuaji wa viwanda endelevu na unaoharakishwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha