Angola yafanya mashauriano ya kikanda kuhusu mvutano kati ya DRC na Rwanda

(CRI Online) Novemba 25, 2022

Rais Joao Lourenço wa Angola ameongoza mkutano wa mashauriano ya kikanda mjini Luanda ili kutafuta ufumbuzi wa mgogoro kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rwanda.

Rais Felix Tshisekedi wa DRC, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, na mratibu wa mazungumzo ya amani aliyeteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta wamehudhuria mkutano huo.

Ajenda kuu ya mkutano huu ni kupitisha mpango kazi wa kurejesha amani nchini DRC na kurekebisha uhusiano kati ya nchi hiyo na Rwanda.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha