China yasema sera yake ya mambo ya nje inasimamia amani na maendeleo ya pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2022

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning Jumanne alisisitiza kwamba sera ya mambo ya nje ya China inasimamia amani na maendeleo ya pamoja.

Msemaji Mao ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kila siku na waandishi wa habari alipojibu swali kuhusu maoni ya Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwenye makala yake iliyochapishwa katika Jarida la Foreign Affairs kwamba kuibuka kimaendeleo kwa China hakumaanishi kuitenga Beijing au kuzuia maendeleo, na kwamba yeye binafsi hakubaliani na muono wa kwamba Vita Baridi vipya vimekaribia.

Msemaji Mao amesema, sera ya mambo ya nje ya China inasimamia amani na maendeleo ya pamoja. Na kwamba China imejitolea kwa ushirikiano wa kirafiki na nchi zote duniani.

“Ukweli umeonesha kwamba maendeleo ya China yanachangia kwenye nguvu ya Dunia kwa ajili ya amani. Yanaongeza nguvu na kuleta fursa kwa ajili ya maendeleo ya Dunia,” msemaji Mao amesema.

Huku akiweka bayana kuwa kuitenga China na kuzuia ushirikiano nayo hakuna manufaa kwa mtu yeyote, Msemaji Mao amesema katika siku hizi, wimbi la utandawazi wa uchumi ni mwelekeo ambao hauwezi kurudishwa nyuma, na Dunia inahitaji ushirikiano zaidi wa kunufaishana.

China imeunganishwa kwa kina katika uchumi wa Dunia na mfumo wa kimataifa, na Dunia haitarudi nyuma kwenye siku za kutengana na mgawanyiko wa pande, Msemaji Mao amesema.

Haiwezekani kwa nchi yoyote kufanikiwa wakati wa kufungwa kwa mlango, amesema, huku akiongeza kuwa kushinikiza kutengwa na kuvuruga minyororo ya viwanda na ugavi na kujenga "ua ndogo zilizo na uzio mrefu" hakumnufaishi yeyote na hatimaye italeta athari mbaya kwa mhusika.

"China haiwezi kupata maendeleo kwa kujitenga na Dunia, na Dunia pia inaihitaji China kwa ajili ya ustawi wake. China itaendelea kufungua mlango kwa kiwango cha juu na kuchangia fursa za maendeleo pamoja na nchi nyingine," Msemaji Mao amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha