Rais Xi Jinping atoa hotuba kwenye maombolezo ya kifo cha Hayati Jiang Zemin

(CRI Online) Desemba 07, 2022

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na rais wa China Xi Jinping aliongoza mkutano wa kuomboleza kifo cha aliyekuwa rais wa China Hayati Jiang Zemin uliofanyika asubuhi tarehe 6 katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Akihutubia mkutano huo, Rais Xi alisifia maisha matukufu ya Hayati Jiang Zemin na mafanikio makubwa aliyoyapata katika utawala wa nchi. Amesisitiza kuwa Hayati Jiang Zemin kupendwa, kuheshimiwa na kukumbukwa na watu wa China kunatokana na kujitolea kwake kwa moyo wote kwa ajili ya watu wa China akifanya juhudi kwa maisha yake yote katika kupigania uhuru, ukombozi na ustawi wa taifa la China na watu wake. Amesema, maendeleo makubwa yaliyopatikana na Chama na taifa la China katika miaka 13 baada ya Mkutano wa nne wa Kamati Kuu ya 13 ya CPC hayawezi kuondokana na uongozi hodari wa Hayati Jiang Zemin akiwa na uwezo mkubwa na maono ya mbali. Hayati Jiang ametoa mchango wa kudumu kwa CPC na watu wa China akipendwa na kuheshimiwa na Chama kizima, jeshi zima, na watu wa makabila yote nchini China na kusifiwa sana na jumuiya ya kimataifa.

Rais Xi amesema kuwa sifa ya Hayati Jiang Zemin pamoja na mafanikio, mawazo na mienendo yake vitaandikwa kwenye kumbukumbu za historia na kukumbukwa daima mioyoni mwa watu wa China kizazi baada ya kizazi. Alitoa wito kwa Chama kizima, jeshi zima na watu wa makabila yote nchini kuunga mkono Kamati kuu ya CPC kwa mshikamano mkubwa zaidi, kusonga mbele kwa ujasiri, na kufungamana zaidi katika juhudi zao za kujenga nchi ya kisasa ya ujamaa na kutimiza ustawi mpya wa taifa la China katika pande zote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha