Meli ya China ya kufuatilia anga ya juu yaanza safari kwa ajili ya misheni mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2022

Picha iliyopigwa kutoka angani ikionyesha meli ya China inayofuatilia vyombo vya anga ya juu ya Yuanwang-3 ikisafiri kwenye eneo la mdomo wa Mto Changjiang wa China, Julai 5, 2019. (Xinhua/Li Yuze)

NANJING - Meli ya ufuatiliaji ya China Yuanwang-3 imeondoka kwenye bandari siku ya Jumapili kwa ajili ya jukumu jipya la ufuatiliaji wa vyombo vya anga ya juu.

Wafanyakazi wa meli hiyo watatumia likizo ya Mwaka Mpya na Sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa China kwenye safari hii. Kabla ya kutia nanga kwa meli, watakuwa wamechunguza vifaa kwenye anga ya juu, kupokea mafunzo, na kujaza vifaa ili kuhakikisha mafanikio ya kazi.

Mwaka huu, meli hiyo imetumia zaidi ya siku 120 baharini, ikisafiri zaidi ya maili 33,000 za baharini, na kukamilisha kazi nne za ufuatiliaji, ikiwa ni pamoja na ile ya chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14.

Yuanwang-3 inawakilisha meli ya kizazi cha pili ya China ya kufuatilia anga ya juu. Inafanya ufuatiliaji wa baharini na ufuatiliaji wa satelaiti za abiti ya juu, kati na ya chini, vyombo vya anga ya juu, na moduli za vituo vya anga ya juu.

Tangu ilipozinduliwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, meli hiyo imefanya zaidi ya safari 60 na kukamilisha misheni 100, ikiwa ni pamoja na kufuatilia vyombo vya anga ya juu vya Shenzhou, uchunguzi wa mwezi wa Chang'e, na satelaiti za BeiDou, na kudumisha kiwango cha mafanikio cha asilimia 100.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha