Rais Xi atumiana salamu za pongezi na gavana mkuu wa New Zealand kwa kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2022

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Alhamisi alitumiana salamu za pongezi na Gavana Mkuu wa New Zealand Cindy Kiro kwa kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Huku akieleza kuwa China na New Zealand ni washirika muhimu, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 50 iliyopita, uhusiano wa nchi hizo mbili umedumisha maendeleo mazuri na utulivu na kuanzisha mambo mengi ya "kwanza".

Ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali umeleta manufaa kwa watu wake na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa kikanda, ameongeza Rais Xi.

Rais Xi pia amesema kwamba anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili, na yuko tayari kushirikiana na Kiro kupitia uzoefu wa kihistoria, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na kusukuma mbele ushirikiano wa kimkakati wa pande mbili za China na New Zealand, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo.

Kwa upande wake, Kiro amesema uhusiano wa New Zealand na China ni moja ya uhusiano muhimu kati ya nchi mbili, na tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 50 iliyopita, mafanikio makubwa yamepatikana katika maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili.

Ameeleza kuwa, New Zealand inathamini historia ndefu ya mazungumzo kati ya nchi hizo mbili, na inatarajia kuendeleza zaidi ushirikiano wa nchi mbili kwa manufaa ya watu wao na Dunia nzima.

Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na mwenzake wa New Zealand, Jacinda Ardern, pia walitumiana salamu za pongezi.

Li amesema, China inatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na New Zealand, na iko tayari kushirikiana na New Zealand kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kama mwanzo mpya wa kuimarisha mawasiliano, kuongeza hali ya kuaminiana, kupanua mabadilishano na kuendeleza ushirikiano ili kusukuma mbele maendeleo mapya na makubwa zaidi ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Katika ujumbe wake, Ardern amesema New Zealand inaiona China kama sehemu muhimu kwa ustawi na utulivu wa kikanda. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha