Xi Jinping atoa hotuba katika mkutano wa Kamati Kuu inayoshughulikia kazi za vijijini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 26, 2022

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, akihudhuria na kuhutubia mkutano wa mwaka wa kamati kuu inayoshughulikia kazi za vijiji uliofanyika Beijing, China kuanzia Desemba 23 hadi 24. (Xinhua/Rao Aimin)

BEIJING - Mkutano wa mwaka wa kamati kuu inayoshughulikia kazi za vijiji nchini China umefanyika kuanzia Desemba 23 hadi 24 hapa Beijing. Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), alihudhuria mkutano huo na kutoa hotuba muhimu. Amesisitiza kuwa huo ni mpango mkakati ambao Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China imeufanya ili kuendeleza ustawishaji wa vijiji kote nchini na kuharakisha ujenzi wa kilimo chenye nguvu, kwa nia ya kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote.

Amesisitiza kuwa nchi ya China lazima kwanza iimarishe kilimo ili kujiimarisha, na pale tu kilimo kinapokuwa na nguvu nchi inaweza kuwa na nguvu. Bila kilimo imara, hakutakuwa na nchi kubwa yenye maendeleo ya kisasa. Maendeleo ya kisasa ya kijamaa hayatakamilika bila maendeleo ya kisasa ya kilimo na vijiji.

Pia ametoa wito kwa kufanyika juhudi katika maeneo yanayohusu kilimo, vijiji na wakulima, lengo kuu likiwa ni ustawishaji wa vijiji, ili kuhimiza kwa dhati maendeleo ya kisasa ya kilimo na maeneo ya vijijini, na kuharakisha ujenzi wa kilimo chenye ustawi mkubwa.

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang aliongoza mkutano huo. Li Qiang, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi na Ding Xuexiang walihudhuria mkutano huo.

Rais Xi ameeleza kuwa kilimo chenye nguvu ni msingi wa nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo. Maendeleo ya kilimo ni muhimu ili kukidhi mahitaji ya watu kwa maisha bora, kufikia maendeleo ya hali ya juu na kuimarisha msingi wa usalama wa taifa.

Rais Xi amesema kuwa kuendeleza ustawishaji wa vijiji kote nchini kazi muhimu katika kujenga kilimo chenye nguvu katika zama mpya, hivyo kuna ulazima wa kuhamishia huko rasilimali watu, rasilimali za nyenzo, na usaidizi wa kifedha.

Kazi lazima ifanyike ili kufufua maeneo matano ikiwa ni pamoja na viwanda, wafanyakazi wenye ujuzi na maarifa, utamaduni, mfumo wa ikolojia, na mashirika katika maeneo ya vijijini kwa njia iliyoratibiwa, huku msisitizo ukiwekwa kwenye sekta kuu na kushughulikia mapungufu.

Rais Xi amesisitiza haja ya kutegemea sayansi na teknolojia pamoja na mageuzi ili kuharakisha ujenzi wa kilimo chenye nguvu. “Tunapaswa kuzingatia mpaka wa sayansi na teknolojia ya kilimo duniani, kukuza kwa nguvu kiwango cha sayansi ya kilimo na teknolojia ya nchi, na kuharakisha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya kilimo na kuwa na uwezo wa kujitegemea na kujiimarisha katika viwango vya juu.”

Huku akisisitiza kuimarisha na kupanua juhudi za mafanikio ya kutokomeza umaskini, Rais Xi amesema kuwa uongozi mzima wa Chama lazima udumishwe kwa uthabiti juu ya kazi zinazohusiana na kilimo, vijiji na wakulima, mfumo wa uongozi na utaratibu wa kufanya kazi lazima uboreshwe, kutoa dhamana thabiti ya kuharakisha ujenzi wa kilimo chenye nguvu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha