Ndege ya China ya C919 yaanza mchakato wa usafiri wa kuthibitishwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 27, 2022
Ndege ya China ya C919 yaanza mchakato wa usafiri wa kuthibitishwa
Ndege kubwa ya abiria ya C919 ikianza kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shanghai Hongqiao huko Shanghai, Mashariki mwa China, Desemba 26, 2022. Ndege kubwa ya abiria ya China C919 imekamilisha safari yake ya kwanza ya kuthibitishwa siku ya Jumatatu, ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Shanghai na kutua kwenye uwanja wa ndege hapa Beijing. Hii inaashiria kuanzishwa kwa mchakato wa kuthibitishwa kwa ndege hiyo kusafiri kwa saa 100, ambao utaendelea hadi katikati ya Februari 2023. Mchakato wa majaribio utathibitisha kwa kina kutegemewa kwa C919 kwa kuzingatia uendeshaji wa kibiashara -- kwa lengo la kuhakikisha usalama na ufanisi wake. (Xinhua)

SHANGHAI - Ndege kubwa ya abiria ya China C919 imekamilisha safari yake ya kwanza ya kutihibitishwa siku ya Jumatatu, ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Shanghai na kutua kwenye uwanja wa ndege hapa Beijing.

Hii inaashiria kuanzishwa kwa mchakato wa kuthibitishwa kwa ndege hiyo kusafiri kwa saa 100, ambao utaendelea hadi katikati ya Februari 2023. Mchakato wa majaribio utathibitisha kwa kina kutegemewa kwa C919 kwa kuzingatia uendeshaji wa kibiashara -- kwa lengo la kuhakikisha usalama na ufanisi wake.

C919 ni ndege kubwa ya kwanza ya abiria kuundwa nchini China.

Shirika la Ndege la China Eastern, waendeshaji wa kwanza wa C919 limesema, Mchakato wa uthibitishaji wa safari ya ndege wa saa 100 utashuhudia ndege hiyo ikitua katika miji kadhaa kote China, ikijumuisha Beijing, Chengdu, Xi'an, Haikou na Qingdao.

Ndege ya kwanza ya C919 iliwasilishwa kwa Shirika la Ndege la China Eastern mapema mwezi huu.

Kundi la kwanza la marubani, wahudumu wa ndege na wafanyakazi wa ukarabati wamemaliza mafunzo yao, na mafunzo zaidi kwa wafanyakazi katika nyadhifa muhimu yamefanywa, Shirika la Ndege la China Eastern limesema.

Matokeo ya mchakato wa uthibitishaji wa safari ya ndege yatakaguliwa kwa makini na Idara ya Usafiri wa Ndege ya China, na kibali cha kufanya kazi kwa ndege ya C919 kitatolewa kwa shirika hilo la ndege ikiwa matokeo ya majaribio yataridhisha.

Ndege hiyo inatarajiwa kuanza kutumika kibiashara na shirika hilo la ndege la China Eastern katika majira ya masika ya Mwaka 2023.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha