Kongamano la “Kutazama Televisheni , Kutazama China” kwa Vijana wa ng’ambo kutathimini na kuchambua Kazi za Filamu za China lafanyika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2023

(Picha ilitolewa na waandalizi.)

Kongamano la “Kutazama Televisheni, Kutazama China” kwa Vijana wa ng’ambo kutathimini na kuchambua Kazi za Filamu za China (tawi la jukwaa la Tanzania) lilifanyika kwa mafanikio kupitia video mchana wa Desemba 29.

Kongamano hilo liliandaliwa na Chuo cha Lugha za Kigeni na Utamaduni katika Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Habari cha China na Kituo cha Utafiti kuhusu Tanzania cha chuo hicho chini ya uongozi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Kimataifa ya Idara Kuu ya Radio na Televisheni ya China, likisaidiwa na kampuni ya Star Times ya Beijing. Kongamano hilo, lilianza kwa kutazama filamu ya rikodi “Maajabu ya Mazingira ya Asili” na washiriki walizungumza na kujadilia kuhusu vijana wa China na Afrika na tafsiri za filamu za China kwa lugha za nchi za Afrika.

Naibu Mkurugenzi wa Chuo cha Lugha za Kigeni na Utamaduni katika Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Habari cha China Liu Ying alihutubia ufunguzi wa kongamano hilo. Liu alisema, katika mabadilishano ya kitamaduni kati ya China na Tanzania, vijana wa nchi hizo mbili si tu ni waliotangua bali pia ni nguvu kuu. Kutazama filamu za televisheni ni njia bora kwa vijana hao kuelewa utamaduni wa nchi hizo na pia kuhimiza maelewano.

Washiriki walitoa hotuba kuhusu mada mbalimbali. Aliyekuwa Konsela wa utamaduni wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Liu Dong alikumbuka historia ya tafsiri za filamu za China kwa lugha za nchi za Afrika; Mkaguzi wa tafsiri za Kiswahli, ambaye alikuwa profesa na mtangazaji wa Kiswahili wa Radio China Kimataifa Bibi Chen Lianying alizungumzia umuhimu wa kuchagua na kutafsiri filamu nzuri za China, na kusisitiza zaidi umuhimu wa kujifunza vizuri lugha ya Kichina, Kiswahili na Kingereza bila kutegemea vyombo vya tafsiri visivyopevuka, ili kupata tafsiri sahihi ya lugha ya Kiswahili na kuwawezesha watazamaji waswahili waelewe na kuijua China vizuri; Mtaalamu wa Kiswahili wa People’s Daily Online Kwizela Aristide Basebya alisema, filamu za China zina uwezo mkubwa wa kukubalika barani Afrika, mambo kama vile utamaduni wa China wenye historia ndefu na mabadilishano ya China na Afrika baada ya kipindi cha ukoloni yanatakiwa kutumiwa zaidi katika maudhui; na kijana mwakilishi kutoka Afrika Tewele Ayubu Damiani alisema, filamu za China zinapendwa na vijana wa Afrika, anatumai kuona filamu nyingi zaidi za Afrika zikitafsiriwa kwa lugha ya Kichina.

Inaelezwa kwamba, Kongamano la “Kutazama Televisheni na Kutazama China ” kwa Vijana wa n’gambo lilianzishwa kwa juhudi za pamoja na Chuo cha Lugha za Kigeni na Utamaduni katika Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Habari cha China, Kituo cha Utafiti kuhusu Pakistan, Kituo cha Utafiti wa BRICS na Kituo cha Utafiti kuhusu Tanzania. Linalenga kusaidia uenezi wa kazi za filamu za televisheni za China kwa vijana wa nchi za nje kwa kupitia dirisha la chuo kikuu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha