Rais Xi Jinping asisitiza juhudi za kufuata njia ya kisasa katika kazi za mahakama, uendeshaji wa mashtaka na usalama wa umma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 09, 2023

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesisitiza umuhimu wa kuendelea kufanya jitihada bila kulegalega katika kuendeleza mageuzi na kutafuta misingi mipya, na kuendeleza moyo wa mapambano katika jitihada za kufuata njia ya kisasa katika kazi za vyombo vya mahakama, uendeshaji wa mashtaka na usalama wa umma.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, hivi karibuni alitoa maagizo muhimu kuhusu kazi ya vyombo vya mahakama, uendeshaji wa mashtaka na usalama wa umma.

Kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC, Rais Xi ametoa salamu na shukrani kwa maafisa wote wa polisi kabla ya Siku ya Polisi ya Umma wa China, ambayo itaadhimishwa Januari 10.

Rais Xi pia amesisitiza kutilia maanani uongozi kamili wa CPC juu ya kazi ya mahakama, uendeshaji wa mashtaka na usalama wa umma, na kuongeza uelewa wa kisiasa pamoja na uwezo wa kisiasa wakuchambua , kufikiri na kutekeleza.

Rais Xi ametoa wito wa kutumia falsafa inayoweka watu mbele na kufuata njia ya sheria ya ujamaa yenye umaalum wa China.

Amesema kuwa, vyombo vya mahakama, uendeshaji wa mashtaka na usalama wa umma vitekeleze wajibu wao wa kuhakikisha usalama wa nchi wa kisiasa, utulivu wa kijamii, usawa na haki za kijamii, maisha ya furaha kwa wananchi, na kutoa mchango katika ujenzi wa nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote na kuendeleza Ustawi wa Taifa la China katika pande zote.

Rais Xi pia amezitaka kamati za CPC katika ngazi zote kuimarisha uongozi juu ya kazi ya mahakama, uendeshaji wa mashtaka na usalama wa umma, ili kutoa hakikisho la kithabiti la kuhimiza kufuata njia ya kisasa katika kazi za mahakama, uendeshaji wa mashtaka na usalama wa umma.

Maagizo hayo ya Xi yametolewa na Chen Wenqing, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mkuu wa Kamati Kuu ya Siasa na Sheria kwenye mkutano mkuu wa kazi za mahakama, uendeshaji wa mashtaka na usalama wa umma uliofanyika Beijing, China kuanzia Jumamosi hadi Jumapili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha