Kituo kikuu cha majaribio ya nishati ya hidrojeni chaanza kufanya kazi Kusini Magharibi mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 11, 2023

Picha iliyopigwa Septemba 16, 2022 ikionyesha gari linalotumia betri ya mafuta ya hidrojeni likionyeshwa kwenye ukumbi wa ndani wa maonyesho ya Mkutano wa 2022 wa Magari Yanayounganishwa na Teknolojia za Akili Bandia Duniani katika Wilaya ya Shunyi, Beijing, China. (Xinhua/Ren Chao)

CHONGQING - Kituo cha Taifa cha Ukaguzi na Upimaji wa Ubora wa Umeme wa Haidrojeni, shirika linalojikita katika kukuza maendeleo ya sekta ya magari yanayotumia nishati ya mafuta ya hidrojeni nchini China, kimeanza kazi Jumatatu mjini Chongqing.

Kikiwa na uwekezaji wa jumla wa Yuan milioni 500 (kama dola za Kimarekani milioni 73.9), kituo hicho kinachukua ukubwa wa eneo la hekta 12.67 na maabara za magari yanayotumia nishati ya hidrojeni, seli za mafuta ya hidrojeni, na uunganishaji wa nishati.

Kituo hicho kinaweza kutoa huduma za majaribio kwa mnyororo mzima wa viwanda, ikijumuisha magari yanayotumia betri za mafuta ya hidrojeni, sehemu muhimu za magari na ubora wa hidrojeni.

Kituo hicho, cha kwanza cha aina yake nchini China, kimeanzishwa na Taasisi ya Utafiti wa Uhandisi wa Magari ya China.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Chongqing ulioko Kusini-Magharibi mwa China umeongeza juhudi za kukuza maendeleo ya tasnia ya magari yanayotumia betri za hidrojeni, na kampuni kadhaa za kutengeneza magari zikitoa modeli mbalimbali za magari na biashara kuu zinazounga mkono kuwekeza huko.

Mji huo umeshirikiana na Mkoa jirani wa Sichuan kujenga "ukanda wa hidrojeni," ambapo karibu magari 1,000 ya vifaa vya mafuta ya hidrojeni yanatarajiwa kuanza kutumika ifikapo Mwaka 2025.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha