Afrika Kusini kutoweka vizuizi vya kusafiri kwa nchi nyingine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 12, 2023

Wasafiri wakiingia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town wa Afrika Kusini, Novemba 29, 2021. (Str/Xinhua)

JOHANNESBURG - Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Joe Phaahla amesema Jumanne kwamba hakuna haja ya kuweka vizuizi kwa nchi nyingine zilizo na maambukizi mengi ya UVIKO-19 kufuatia kugunduliwa kwa virusi vipya vya Korona jamii ya Omicron XBB.1.5 nchini mwake.

"Hatukuwa tukiweka vizuizi vyovyote au mahitaji ya kusafiri kwa China, Marekani au nchi yoyote iliyo na maambukizi yanayoongezeka," Phaahla amesema wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu UVIKO-19.

Mgonjwa aliye na maambukizi ya virusi vya Korona jamii ya XBB.1.5 aligunduliwa Desemba 27 wakati wa kuchukuliwa sampuli kinasibu na maelezo zaidi bado hayajulikani, amesema.

Waziri huyo amesema wameshirikisha wanasayansi, Shirika la Afya Duniani na kamati ya ushauri ya mawaziri, ambao wamependekeza kwamba hakuna haja ya kuweka vizuizi vya kusafiri ndani au kwa nchi yoyote.

“Tulishauriwa kuongeza ufuatiliaji na chanjo, tutafanya upimaji wa maji machafu kwenye ndege kutoka China, Marekani au nchi yoyote yenye maambukizi yanayoongezeka ili kuangalia virusi hivyo, tutaongeza mawasiliano na mtangazo ili watu wapate chanjo au kudungwa dozi za nyongeza," amesema.

Michelle Groome, ofisa katika Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Kuambukiza nchini humo, amesema upimaji wa maji machafu kwenye ndege utaanza wiki ijayo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha