Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa azitaka nchi wanachama kudumisha dira na maadili ya Umoja wa Mataifa hasa utekelezaji wa sheria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 13, 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (katikati, mbele) akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu mfumo wa uhusiano wa pande nyingi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Desemba 14, 2022. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Alhamisi ametoa wito kwa nchi zote wanachama kudumisha dira na maadili ya Katiba ya Umoja wa Mataifa na hasa utekelezaji wa sheria.

"Kwanza kabisa, naziomba nchi zote wanachama kudumisha dira na maadili ya Katiba ya Umoja wa Mataifa na Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu, na kufuata sheria za kimataifa," mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameuambia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ukuzaji na uimarishaji wa utekelezaji wa sheria katika kudumisha amani na usalama wa kimataifa.

Akibainisha kwamba utekelezaji wa sheria ni "msingi wa Umoja wa Mataifa, na dhamira yetu ya amani," na kwamba msingi wa utekelezaji wa sheria ni kwamba "watu wote, taasisi, na vyombo, vya umma na vya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na serikali yenyewe, wanawajibika mbele ya sheria," ofisa huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema utekelezaji wa sheria unalinda watu walio hatarini, na kuzuia ubaguzi, unyanyasaji na uvunjifu mwingine wa haki za binadamu.

"Ni mstari wetu wa mbele wa ulinzi dhidi ya uhalifu wa ukatili, ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki. Unajenga na kuimarisha imani kwa taasisi. unaunga mkono haki, uchumi na jamii jumuishi. Na ni msingi wa ushirikiano wa kimataifa na ushirikiano wa pande nyingi," amesema.

"Tuko katika hatari kubwa ya Utawala wa Uasi," ameonya Guterres.

Picha hii iliyopigwa Septemba 14, 2020 ikionyesha bendera ya Umoja wa Mataifa ikipepea nje ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. (Xinhua/Wang Ying)

“Nategemea nchi wanachama ziunge mkono juhudi zetu za kuhimiza utekelezaji wa sheria katika pande zote,” ameongeza.

Amesema, ingawa changamoto ni nyingi, utekelezaji wa sheria ni muhimu zaidi kwa kudumisha amani na usalama wa kimataifa na kwa juhudi za kujenga amani. "Ninaziomba nchi wanachama kutumia kikamilifu utekelezaji wa sheria kama chombo cha kuzuia."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha