Kampuni ya China kukamilisha mradi wa umeme wa Konza wa Kilovati 400 katika Mji wa teknolojia mahiri wa Kenya mwishoni mwa Oktoba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 17, 2023

NAIROBI - Kampuni ya China Aerospace Construction Group (CACGC) imepanga kukamilisha ujenzi wa kituo kidogo cha Konza cha kubadilisha umeme kwa Kilovati 400 na kuunganisha njia za juu za kusambaza umeme katika eneo la Mji wa Teknolojia wa Konza, ambao ni mji wa teknolojia mahiri wa Kenya, ifikapo mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.

Zhu Yunye, Meneja wa Mradi wa Upanuzi wa Usambazaji Umeme wa Kenya (KPTEP), amesema kuwa ujenzi wa njia ya kusambaza umeme yenye urefu wa Kilomita 40, na nguvu za Kilovati 400 kutoka Isinya hadi Konza na vituo vidogo vinavyohusika kwa sasa umekamilika kwa asilimia 70.

"Pia tumekusanya karibu asilimia 95 ya nyenzo na vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya ufungaji wa mradi," Zhu ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Kituo hicho kidogo cha Konza cha kubadilisha umeme kwa Kilovoti 400, kilichoko takriban umbali wa kilomita 70 Kusini mwa Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi, ni sehemu ya mradi wa KPTEP ambao unafadhiliwa na Benki ya Exim ya China, Zhu amesema.

Hu Jing, mwakilishi mkuu wa CACGC nchini Kenya amesema kuwa CACGC ina nia ya kuingiza teknolojia za kisasa za China katika sekta ya usambazaji wa umeme wa juu barani Afrika na imejitolea kufanikisha mradi huo wa KPTEP.

"Wakati wa utekelezaji, mradi wa KPTEP umekuwa ukitoa mafunzo na kutoa nafasi zaidi ya 1,000 za kazi kwa jamii za wenyeji," amesema.

Alex Wachira, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya, amesema kuwa kampuni hiyo ya China ina uwezo wa kutekeleza mradi huo ndani ya muda uliopangwa kulingana na mkataba.

Wachira amesema kuwa mradi huo ni muhimu sana kwa Kenya kwa sababu utatoa nishati ya kutosha na ya kutegemewa kwa teknolojia, ambayo ni moja ya miradi kinara ya maendeleo nchini humo.

"Mradi huo pia utawezesha viwanda vikubwa vya ndani na nje kuanzishwa katika mji huo wa teknolojia mahiri," ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha