Xi Jinping awataka wajumbe wasio wanachama wa CPC wakusanye nguvu za kutumikia maslahi ya jumla ya nchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 17, 2023

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Xi Jinping, ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihudhuria kwenye mkutano wa kila mwaka wa kujumuika pamoja na wajumbe wasio wa Chama cha CPC kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Januari 16, 2023. Wang Yang, Wang Huning na Ding Xuexiang pia walihudhuria mkutano huo. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Jumatatu ametoa wito kwa wajumbe wasio wanachama wa CPC kutekeleza majukumu yao kwa juhudi na dhamira kufanya kazi kubwa zaidi katika kuwashirikisha watu na kutumikia maslahi ya jumla ya nchi.

Xi aliyasema hayo alipohudhuria kwenye mkutano wa kila mwaka wa kujumuika pamoja na wajumbe wa vyama visivyotokana na CPC kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

Kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Rais Xi ametoa pongezi kwa viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni wa kamati kuu za vyama vinane vya kidemokrasia na Shirikisho la Viwanda na Biashara la China (ACFIC), na kutuma salamu kwa watu wasio na chama, na wajumbe wa umoja wa mstari wa mbele.

Mwaka 2023 ni mwaka wa kwanza wa kusoma na kutekeleza mipango na misingi ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, huku kukiwa na matumaini na changamoto kwa pamoja, Rais Xi amesema, huku akitoa wito kwa juhudi za pamoja za kuendeleza maendeleo ya mambo ya kisasa ya China.

Rais Xi alitoa hotuba muhimu katika mkutano huo. Amesema Mwaka 2022 ulikuwa muhimu sana katika historia ya maendeleo ya Chama na nchi. Mwaka huo pia uliadhimisha miaka 100 ya Chama kutambulisha kwa uwazi sera yake ya umoja wa mstari wa mbele.

Rais Xi amesisitiza kuwa kushikilia uongozi wa CPC na kuungana kwa unyoofu bila kuyumbayumba na kufanya kazi pamoja na CPC ndiyo kanuni ya msingi wa kisiasa wa ushirikiano wa vyama vingi chini ya uongozi wa Chama cha CPC.

Rais Xi amesema kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya mambo ya kisasa katika pande zote na kuendeleza ustawi wa Taifa la China katika sekta zote kunahitaji juhudi za pamoja za watu wote nchini China. Rais Xi pia ametoa wito kwa vyama vya kidemokrasia kufanya kazi kama washauri wazuri, wasaidizi, na wenzake wa CPC.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha