Mwitikio ulioboreshwa wa China wa kukabiliana na UVIKO kusaidia ufufukaji wa uchumi wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 18, 2023

Picha hii iliyopigwa Januari 10, 2023 ikionyesha daraja la Mto Haihe, njia muhimu ya usafirishaji wa mizigo, katika Eneo Jipya la Binhai, Tianjin Kaskazini mwa China. Shughuli za kijamii na kiuchumi za watu polepole zinarejea katika hali ya kawaida baada ya China kuboresha hatua zake za kukabiliana na UVIKO-19. (Xinhua/Zhao Zishuo)

BEIJING - Kadiri hali ya jumla ya udhibiti wa maambukizi ya UVIKO-19 inavyoimarika na maisha na kazi kurejea katika hali ya kawaida kwa kasi ya haraka, uhai wa kiuchumi na kijamii na maendeleo ya China yatapatikana kikamilifu, jambo ambalo litaongeza imani na nguvu zaidi katika kufufuka kwa uchumi wa Dunia, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin amesema Jumanne.

Kauli ya msemaji huyo inakuja wakati Katibu Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) Mathias Cormann alisema Jumatatu kwamba hakika anakaribisha sana kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa hatua zinazohusu UVIKO nchini China, ambayo ni nzuri sana katika kuhakikisha kuwa minyororo ya ugavi inafanya kazi kwa uwezo wake na ufanisi zaidi na itasaidia kupunguza mfumuko wa bei.

"Tumeona ripoti husika. Tumeona pia kwamba hivi majuzi, taasisi nyingi zaidi za kitaalamu za kimataifa zimesema kwamba kuboresha kwa China kwa hatua za kukabiliana na UVIKO-19 kutaonesha kusaidia uchumi wa dunia," Wang amesema kwenye mkutano wa kila siku na waandishi wa habari.

Borge Brende, Rais wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF), amesema katika siku za hivi karibuni kwamba uboreshaji wa China wa hatua za kukabiliana na UVIKO-19 utasababisha ukuaji wa uchumi wenye nguvu na ustawi zaidi na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Dunia.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limebainisha kuwa China itafikia lengo la ukuaji thabiti wa uchumi Mwaka 2023 na kuwa sababu za kuleta hamasa zaidi kwa uchumi wa Dunia.

Benki nyingi za kimataifa za uwekezaji na taasisi za fedha zikiwemo Morgan Stanley, Goldman Sachs, HSBC, Barclays na Natixis zimerekebisha makadirio yao ya kiwango cha ukuaji wa uchumi wa China Mwaka 2023.

"Serikali ya China imechukua hatua ya kurekebisha hatua zake za kukabiliana na UVIKO kwa kuzingatia hali ya hivi sasa. Hii ni hatua sahihi katika kuratibu kikamilifu mwitikio wa janga na maendeleo ya kijamii na kiuchumi," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha