Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine afariki katika ajali ya helikopta

(CRI Online) Januari 19, 2023

Helikopta ilianguka karibu na mji wa Kiev Jumatano asubuhi, na kusababisha vifo vya takriban watu 16, akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine Denys Monastyrsky.

Idara ya Huduma ya Dharura ya Taifa ya Ukraine imesema ajali hiyo iliyotokea katika mji wa Brovary katika vitongoji vya Kiev, pia ilisababisha kifo cha naibu wa Monastyrsky, Yevhen Yenin na wengine 30 kujeruhiwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha