Naibu waziri mkuu wa China afanya mazungumzo na waziri wa fedha wa Marekani

(CRI Online) Januari 19, 2023

Naibu waziri mkuu wa China Liu He, ambaye pia ni kiongozi wa upande wa China kwenye mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani Jumatano alifanya mazungumzo na waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen nchini Uswisi.

Zikizingatia utekelezaji wa makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa China na Marekani kwenye mkutano wa Bali, pande hizo mbili zilijadili masuala ya hali ya kiuchumi na kifedha ya nchi hizo mbili na dunia nzima, pamoja na kushughulikia changamoto za pamoja duniani.

Pande mbili ziliona kuwa ufufukaji wa uchumi wa dunia uko katika kipindi muhimu, hivyo zinatakiwa kuimarisha mawasiliano na uratibu juu ya sera, na kushughulikia changamoto za kiuchumi na kifedha kwa pamoja, kitendo ambacho kitazinufaisha China na Marekani na dunia nzima.

Mbali na hayo, upande wa China pia ulieleza wasiwasi wake juu ya sera za kiuchumi, kibiashara na kiteknolojia za Marekani kwa China na kutarajia kuwa Marekani itatilia maanani athari zinazotokana na sera hizo kwa pande zote mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha