Tanzania yadhamiria kuwa kitovu cha biashara ya mtandao barani Afrika

(CRI Online) Januari 20, 2023

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania Bw. Nape Nnauye amesema kuwa Tanzania inawekeza kwa kiasi kikubwa katika teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ikiwemo ujenzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ili kuifanya kuwa kitovu cha biashara ya mtandaoni barani Afrika.

Nnauye amesema hayo katika maadhimisho ya kila mwaka ya Siku ya Posta barani Afrika yaliyofanyika mjini Dodoma.

Aidha, amesema serikali imetunga sheria, kanuni na taratibu za kusimamia biashara ya mtandaoni.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) Bw.  Emmanuel Mannaseh amesema kuwa mamlaka hiyo itaendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha vijana kushiriki katika uchumi wa kidijitali. Amewataka vijana kutumia fursa zinazotokana na teknolojia ya kidijitali ili kuboresha ustawi wao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha