Mashirika ya kibiashara ya Zimbabwe kuandaa kongamano la kuwezesha uhusiano wa biashara na China

(CRI Online) Januari 20, 2023

Mashirika ya kibiashara, utalii na uwekezaji ya Zimbabwe yanapanga kuandaa kongamano la biashara kwa ajili ya kuwezesha biashara na uwekezaji na China.

Mkurugenzi mwendeshaji wa shirika la kukuza biashara la Zimbabawe, ZimTrade, Similo Nkala amesema China imekuwa mshirika muhimu wa Zimbabwe, na juhudi zaidi zitafanywa ili kupiga chapuo uhusiano kati ya nchi mbili.

Nkala amesema Zimbabwe itaongeza shughuli za kurahisisha biashara na kupanua upatikanaji wa bidhaa zake kwenye masoko tofauti kama vile ya China, Malaysia na Misri.

Akitolea mfano China, Nkala amesema ikiwa kama mwagizaji mkubwa na kujivunia kwa kuwa na watu wengi, soko hili linakuwa moja ya masoko makuu ya uagizaji ya Zimbabwe, na tayari linashika nafasi ya tatu kwa kuwa mwagizaji mkubwa wa bidhaa za Zimbabwe.

China ilisaini mkataba na Zimbabwe wa kununua machungwa Mwaka 2022, na kuyapa fursa makampuni ya nchi hiyo kusafirisha machungwa nchini China, ambayo ni moja ya nchi zenye watumiaji wakubwa wa bidhaa za machungwa duniani. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha