Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia azishutumu nchi za Magharibi kwa kuchangia mgogoro wa Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 20, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov akifanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu ufanisi wa diplomasia ya Russia kwa Mwaka 2022 mjini Moscow Januari 18, 2023. (Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia)

MOSCOW - Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov amesema Jumatano kwamba mgogoro wa Ukraine ni "matokeo ya maandalizi ya Marekani na satelaiti zake kwa ajili ya kuanzisha vita mseto duniani dhidi ya nchi yake”.

Nchi za Magharibi zinajaribu kuthibitisha kwamba hazipigani na Russia bali zinaisaidia tu Ukraine kujibu "uchokozi" na kurejesha ukamilifu wa ardhi yake, Lavrov amesema kwenye mkutano wake wa kila mwaka na waandishi wa habari, huku akiongeza kuwa kiwango cha uungaji mkono wao kinaweka wazi kuwa nchi za Magharibi zimewekeza kwa kiasi kikubwa katika vita vyake dhidi ya Russia.

Kuhusu matarajio ya mazungumzo kati ya Russia na nchi za Magharibi juu ya suala la Ukraine, Lavrov amesema kuwa Russia iko tayari kuzingatia kwa makini mapendekezo mazito, lakini hayajatolewa hadi sasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha