Rais Xi Jinping atoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa 7 wa Nchi za Latini Amerika na Karibiani (CELAC)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2023

Kutokana na mwaliko wa Rais Alberto Fernandez wa Argentina, ambaye ni rais wa zamu wa Jumuiya ya Latini Amerika na Karibiani (CELAC), Rais wa China Xi Jinping ametoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Saba wa wakuu wa nchi za CELAC. Mkutano huo umefanyika Buenos Aires, Mji Mkuu wa Argentina, Januari 24, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Mkutano wa Saba wa Kilele wa Jumuiya ya Nchi za Latini Amerika na Karibiani (CELAC) umefanyika Jumanne huko Buenos Aires, Mji Mkuu wa Argentina. Kutokana na mwaliko wa Rais Alberto Fernandez wa Argentina, ambaye ni rais wa zamu wa CELAC, Rais wa China Xi Jinping ametoa hotuba kwa njia ya video kwenye mkutano huo.

Rais Xi amebainisha kuwa nchi za Latini Amerika na Karibiani (LAC) ni sehemu muhimu ya nchi zinazoendelea. Pia ni nchi washiriki na wanaochangia kwa juhudi usimamizi wa kimataifa. Amesema, CELAC imekua kwa kasi na kuwa nguvu muhimu inayosukuma mbele ushirikiano wa kimataifa wa Kusini-Kusini. Pia, CELAC imekuwa na mchango muhimu katika kulinda amani ya kikanda, kukuza maendeleo ya pamoja na kuendeleza ushirikiano wa kikanda.

Rais Xi amesisitiza kuwa China daima inaunga mkono mchakato wa ushirikiano wa kikanda wa Latini Amerika na Karibiani.

"Tunathamini sana uhusiano wetu na CELAC, na tunaichukulia CELAC kama mshirika mwenzi wetu mkuu katika kuimarisha mshikamano kati ya nchi zinazoendelea na kuendeleza ushirikiano kati ya Kusini na Kusini. Ndiyo maana China imekuwa ikishirikiana na nchi za LAC ili kuimarisha kwa kasi Jukwaa la China na CELAC na kuendeleza Uhusiano wa China na LAC kwenye hali ya usawa, yenye manufaa kwa pande zote, uvumbuzi, uwazi na manufaa kwa watu katika zama mpya," amesema.

Rais Xi amesema nchi nyingi zaidi za eneo hilo zimeshiriki katika ushirikiano wa kiwango cha juu wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na China, kuunga mkono na kushiriki katika Pendekezo la Maendeleo ya Dunia na Pendekezo la Usalama wa Dunia , na kushirikiana na China katika kujenga jumuiya ya China na LAC yenye mustakabali wa pamoja.

Amesisitiza kuwa Dunia iko katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko. "Tunaweza tu kukabiliana na changamoto na wimbi la wakati huu kupitia mshikamano mkubwa na ushirikiano wa karibu," amesema.

Ameongeza kuwa China iko tayari kuendelea kushirikiana na nchi za LAC ili kusaidiana na kuhimiza maendeleo kwa pamoja, na kutetea "amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru" – ambayo ni maadili ya pamoja ya binadamu.

Kutokana na mwaliko wa Rais Alberto Fernandez wa Argentina, ambaye ni rais wa zamu wa Jumuiya ya Latini Amerika na Karibiani (CELAC), Rais wa China Xi Jinping ametoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Saba wa wakuu wa nchi za CELAC. Mkutano huo umefanyika Buenos Aires, Mji Mkuu wa Argentina, Januari 24, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha