China yarekodi safari za abiria milioni 226 katika likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 29, 2023

Abiria akiweka mizigo yake kwenye rafu ya juu ndani ya treni katika Stesheni ya Reli ya Shapingba, Chongqing, Kusini Magharibi mwa China, Januari 27, 2023. (Xinhua/Wang Quanchao)

BEIJING - Takriban safari za abiria milioni 226 zimefanywa wakati wa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China iliyohitimishwa Ijumaa wiki hii, takwimu rasmi za serikali zimeonyesha Jumamosi.

Wakati wa likizo hiyo ya siku saba, ambayo ilianza Januari 21 hadi 27, idadi ya safari za watu kwenye njia za reli na barabara ilifikia milioni 50.17 na milioni 162, wakati idadi ya safari za watu zilizofanywa kwa njia za meli na ndege ilifikia karibu milioni 4.87 na milioni 9.01.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ni sikukuu muhimu zaidi nchini China, na vile vile ni wakati muhimu kwa familia kujumuika pamoja na kusafiri. Sikukuu hii kwa mwaka huu iliangukia Januari 22.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha