Mwaka Mpya wa Jadi wa China 2023 yakaribishwa kwa furaha -- Kujumuisha sekta muhimu za Soko la Utamaduni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 01, 2023

Picha iliyopigwa Januari 24 ikionesha wakazi wakisubiri kuingia kwenye ukumbi wa sinema huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning wa China. (Xinhua/Yang Qing)

Katika wakati wa likizo iliyopita ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, matumizi katika ununuzi yalipanda kwa kasi, soko la China limepata nguvu tena, na imani ya kibiashara imeongezeka. Soko la kitamaduni kote nchini China limekaribisha "mwanzo mzuri".

Soko la likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China lilikuwa na hali motomoto

Kuanzia mwanzoni mwa mwaka mpya, soko la filamu la China lilirejea katika hali ya kuwavutia watazamaji filamu.

Kwa mujibu wa takwimu za Idara ya Taifa ya Filamu ya China, jumla ya mauzo ya tiketi kwa ajili ya kutazama filamu kwenye majumba ya sinema wakati wa likizo hiyo, ilifikia yuan bilioni 6.758, ikishika nafasi ya pili katika historia ya kutazama filamu wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

Takwimu za Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China zinaonesha kwamba, wakati wa likizo hiyo, watalii milioni 308 walisafiri ndani ya nchi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23 kuliko lile la mwaka jana, jumla ya mapato yatokanayo na utalii wa ndani yalifikia yuan bilioni 375.843, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 30.

Picha iliyopigwa Januari 25 ikionesha watalii wakitembelea "Soko la Mwaka Mpya Kwenye Maji" katika Eneo la Mandhari la Wuzhen lililoko Mji wa Tongxiang, Mkoa wa Zhejiang nchini China (Xinhua, Huang Zongzhi)

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utalii ya China Bw. Dai Bin, anaamini kwamba kujitokeza kwa kasi kwa mahitaji ya usafiri kama vile kuwatembelea jamaa na marafiki na kusafiri wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China baada ya kukumbwa na janga la virusi vya Korona kumejenga msingi imara wa soko kwa uchumi wa utalii wa mwaka mzima.

Picha iliyopigwa Januari 18 ikionesha washiriki wa Timu ya Wacheza Dragoni wa Moto ya Tongliang wakicheza mchezo wa Dragoni wa Moto wa Tongliang kwenye bustani ya Longcheng Tianjie katika Wilaya ya Tongliang, iliyoko Chongqing, China. (Xinhua, Liu Chan)

Shughuli zilijazwa na umaalumu wa Kichina

Kufurahia kutazama taa za kijadi na kutembelea kwenye masoko ni moja ya shughuli zilizovutia watu sana. Takwimu zinaonyesha kwamba wakati wa likizo hiyo muhimu kwa Wachina ya kila mwaka, takriban jumla ya shughuli 110,000 za kitamaduni zilifanyika kote nchini China, zikihusisha washiriki wapatao milioni 473.

Picha iliyopigwa Januari 25 ikionesha wananchi wakitazama onyesho la kipekee la opera ya Sichuan ya "kubadilisha uso" kwenye Uwanja wa Utamaduni wa “Mji wa Karne” , katika Mtaa wa Huayang wa Eneo la Jiangyang la Mji wa Luzhou mkoani Sichuan, China. (Xinhua/Liu Xueyi)

"Kurudishwa kwa shughuli za kijadi kwa kufuata mila na desturi kunamaanisha matarajio ya kiroho ya watu na imani ya kitamaduni katika sikukuu za jadi za China." Amesema Li Xiangzhen, profesa msaidizi katika Chuo cha Sosholojia cha Chuo Kikuu cha Wuhan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha