Watu nchini China wafanya juhudi wakati wa majira ya kujiandaa kwa kilimo yawadia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 01, 2023

(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)

Kufanya vizuri maandalizi ya kazi ya kilimo katika majira ya mchipuko ni ufunguo wa kuhakikisha uzalishaji na ugavi wa nafaka na bidhaa muhimu za kilimo wa mwaka mzima. Katika siku za hivi karibuni, wakulima kote nchini China wanashiriki kikamilifu katika maandalizi ya uzalishaji wa kilimo, na kuna hali ya kuwepo kwa shughuli nyingi za watu wanaofanya kazi kwa juhudi kubwa mwanzoni mwa majira ya mchipuko.

Maandalizi ya kilimo cha majira ya mchipuko kila mahali

"Tulianza biashara siku ya tatu ya mwezi wa kwanza mwaka huu." Anasema Ren Yuanyuan, muuzaji wa vifaa vya kilimo katika Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini mwa China.

Amesema kwamba wakulima sasa wana uelewa zaidi wa ununuzi wa vifaa vya kilimo kwa wakati unaofaa, na uagizaji wa mapema siyo tu hupunguza gharama, lakini pia huzuia “msongamano” wa ununuzi wakati wa msimu wa kilele wa maandalizi ya kilimo.

Amesema kwamba, wakulima wengi wamelipa mapema amana ya kununua vifaa vya kilimo kuanzia mwezi Oktoba mwaka jana, na kupitia biashara yake hiyo wanaweza kupeleka bidhaa kwenye makazi ya wakulima wakati wowote wakulima wanapopiga simu kwenye duka lake kabla ya msimu wa kupanda mimea mwaka huu.

Kutoka mashamba yenye rutuba ya Kaskazini-Mashariki mwa China hadi Tambarare za Kaskazini za China, idadi kubwa ya wakulima na wafanyakazi wa sekta ya kilimo wanapanga mapema uzalishaji wa nafaka, wakiweka imani yao katika “mashamba ya matumaini”.

(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)

Teknolojia yahimiza kupaa kwa kilimo cha kisasa

 

(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)

Katika maandalizi ya kazi ya kilimo ya majira ya mchipuko ya mwaka huu, nguvu ya sayansi na teknolojia imeleta matumaini makubwa kwenye mashamba.

Katika kitengo cha upandikizaji wa miche cha eneo la uzalishaji wa mbegu la Kampuni ya Hainan Nongle Nanfan, mifumo mingi ya ukuzaji miche imefanywa kwa mashine. Kwa mujibu wa ripoti, uwezo uzalishaji wa mashine kwenye eneo hilo umefikia 80%.

"Mashine zimepunguza gharama za uzalishaji, na ruzuku kwa ajili ya kupanda nafaka imeongeza imani ya upandaji," amesema mkulima Sun Jianhua. 

(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha