Rais Xi asisitiza juhudi katika kuharakisha uanzishaji wa muundo mpya wa maendeleo wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2023

BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesisitiza juhudi za kuharakisha uanzishaji wa muundo mpya wa maendeleo wa China na kuimarisha mipango ya usalama na maendeleo.

Rais Xi ameyasema hayo aliposhiriki kwenye semina elekezi ya pili ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 20 ya CPC Jumanne mchana.

Amesema kuharakisha uanzishaji wa muundo mpya wa maendeleo ni uamuzi wa kimkakati wa kutimiza Lengo la Pili la Miaka 100 na kuhakikisha maendeleo na usalama, pamoja na mpango mkakati wa kuchukua hatua za maendeleo ya baadaye.

“Licha ya maendeleo yaliyopatikana katika baadhi ya kazi za kuanzisha muundo mpya wa maendeleo, bado kuna safari ndefu kabla ya kukamilishwa kwa muundo mpya wa maendeleo ”, Rais Xi amesema, huku akitoa wito wa kushikilia mwelekeo na mtazamo wa mifumo ili kutatua migongano na matatizo makubwa yaliyozuia kazi ya kuharakisha kuanzisha muundo mpya wa maendeleo, kuendeleza kwa kina mageuzi, na kuendeleza uvumbuzi.

Rais Xi amesisitiza kustawishwa kwa mfumo jumuishi wa mahitaji ya ndani ya nchi, unaozingatia upanuzi wa matumizi katika ununuzi inayoungwa mkono na mapato ya watu, mahitaji ya uwekezaji na mapato ya kuridhisha, na mahitaji ya mikopo yenye ukomo katika kiwango na deni.

Rais Xi amesema muundo mpya wa maendeleo unapaswa kuanzishwa kwenye msingi wa mfumo wa viwanda vya kisasa, na mzunguko mzuri wa kiuchumi unahitaji muunganisho wenye utaratibu na ufanisi mzuri kati ya viwanda mbalimbali.

“Nchi itaendelea kuweka mkazo katika maendeleo ya kiuchumi yanayolenga uchumi halisi na kuchukua hatua madhubuti ili kuhimiza maendeleo ya aina mpya ya viwanda ,” ameongeza.

Pamoja na kusisitiza uwiano kati ya maendeleo ya miji na vijiji , Rais Xi ameelezea haja ya China kuendelea na lengo la kufungua mlango kwa kiwango cha juu, haswa katika kuchangia maendeleo ya kiwango cha juu ya ujezi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kushiriki kikamilifu katika mazungumzo yanayohusu sheria na kanuni za uchumi na biashara za kimataifa ili kusaidia kuanzisha utaratibu wa uchumi wa Dunia ulio wa uwazi, anuai na tulivu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha