China yaongeza Maeneo muhimu 18 ya Ardhi Oevu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 03, 2023

Kundi la ndege wenye uso mweusi wakionekana kwenye ardhi oevu ya Ghuba ya Danzhou Mkoani Hainan, Kusini mwa China tarehe 13, Desemba, 2022. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

Tarehe 2, Februari mwaka huu ni Siku ya 27 ya Ardhi Oevu Duniani. Habari kutoka Idara ya Misitu na Mbuga ya China zinasema, China imeongeza maeneo 18 ya ardhi oevu, yakiwemo Ziwa Mabata Pori la eneo la Yanqing la Beijing, Ghuba ya Jiuqushiba ya Daxinganling Mkoani Heilongjiang, Ziwa Baima la Mji wa Huaian Mkoani Jiangsu na nyinginezao, maeneo hayo ya ardhi oevu yamethibitishwa kufuata vigezo vya kutathimini vya “Mkataba wa Ardhi Oevu Muhimu wa Kimataifa” . Kwa jumla sasa kuna maeneo 82 ya ardhi oevu nchini China, na maeneo hayo yamefikia hekta milioni 7.647, ambayo yanachukua nafasi ya nne duniani.

Kaulimbiu ya Siku ya Ardhi Oevu Duniani ya mwaka huu ni “Kurejesha Maeneo ya Ardhi Oevu”. Siku hiyo, China ilifanya shughuli za uenezi kwenye eneo la Xixi la mji wa Hangzhou Mkoani Zhejiang, China.

Katibu mkuu wa “Mkataba wa Ardhi Oevu” Musonda Mumba alipotoa risala kwa shughuli hiyo kupitia video, alishukuru juhudi za uongozi za China ikiwa nchi mwenyeji na nchi mwenyekiti wa Mkutano wa 14 wa Nchi zilizosaidia Mkataba.

Habari zimesema, tangu China iliposaini “Mkataba wa Ardhi Oevu” mwaka 1992, nchi hiyo imerejesha maeneo ya ardhi oevu zilizovia kwa hekta laki 4.674 , na kuongeza maeneo ya ardhi oevu kwa hekta laki 2.026.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha