

Lugha Nyingine
Wanawake wa Tanzania waanzisha tena maisha baada ya kupona kutoka kwenye maradhi ya fistula ya kizazi
Msimamizi wa Kituo cha Mabinti Maria Peter akiongea wakati akihojiwa na Shirika la Habari la China Xinhua kwenye Hospitali ya CCBRT huko Dar es Salaam, Tanzania Februari 3, 2022. (Herman Emmanuel/Xinhua)
Wanawake saba waliopona kabisa kutoka tiba ya maradhi ya fistula ya kizazi wamekua katika mihangaiko chumbani wakitengeneza mabegi yenye ubora. Tokea mwaka 2009, wanawake hao wamekuwa wakipewa mafunzo kwenye Kituo cha Mabinti, ambacho kinaendeshwa chini ya Hospitali ya CCBRT huko Dar es Salaam, ili kuwawezesha wanawake wanaopona kutoka kwenye upasuaji wa fistula kupata stadi za ufundi na za ujasiriamali, ili waweze kuanzisha biashara zao wenyewe.
Tangu CCBRT ilipoanzishwa kama mtoaji wa huduma ya uponyaji kwenye msingi wa makazi, imekuwa mtoaji mkubwa zaidi wa huduma za watu wenye ulemavu na uponyaji katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Mariam Bakari Sobo mwenye umri wa miaka 30 alijiunga kwenye kituo hicho Mei, 2019, akahitimu Desemba, 2019.
“Tangu nilipoajiriwa hapa, nimepata cherehani, na nimeanzisha biashara yangu ndogo nyumnbani nikiwa ni mshonaji, ambayo inanipa kipato cha ziada cha kuhudumia familia yangu,” alisema Sobo.
Maradhi ya fistula ya kizazi ni magonjwa yanayohusika na uzazi. CCBRT inasema, “wanawake wenye magonjwa hayo hutelekezwa na familia na kukataliwa na jamii, wakilazimika kuishi na aibu na kwa kujitenga.”
Msimamizi wa kituo hicho Maria Peter alimwambia mwandishi wa habari kuwa, tangu kituo hicho kilipoanzishwa, kimefundisha wanawake zaidi ya 170 waliopona kutoka maradhi ya fistula ya kizazi.
Kwa wastani kila mwaka CCBRT inatibu wanawake zaidi ya 100 wenye maradhi ya fistula ya kizazi, lakini wanawake wapatao 3,000 huugua maradhi ya fistula ya kizazi kila mwaka nchini Tanzania.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma