

Lugha Nyingine
EAC yapitia tena miradi inayotekelezwa na Tume ya Bonde la Ziwa Victoria
Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta wa Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya hewa la Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ulifunguliwa Jumatatu mjini Bujumbura, Burundi na utapitia tena miradi na programu zinazotekelezwa na Tume ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC).
LVBC ilianzishwa na EAC Mwaka 2001, kama mfumo wa kuratibu masuala mbalimbali yanayohusu ziwa hilo na bonde lake, pia ni kituo cha kuhimiza uwekezaji na kubadilishana taarifa kwa wadau husika.
Taarifa iliyotolewa na makao makuu ya EAC imesema mkutano huo pia utapitia tena miradi ya mamlaka ya usalama wa usafiri wa anga na eneo linalounganishwa kwa mawasiliano ya simu za mkononi. Zaidi ya hayo, wadau watajadili changamoto za maendeleo ya miundombinu, na kutoa mapendekezo juu ya kukabiliana na changamoto hizo kwenye mkutano huo unaofanyika kuanzia Tarehe 6 hadi 10 Mwezi Februari.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma