Huduma za usambazaji wa vifurushi nchini China zaongezeka kwa kasi Mwaka 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 10, 2023

Wafanyakazi wa kampuni za utoaji wa huduma za usambazaji wa vifurushi wakifanya kazi kwenye Soko la Maua la Kunming Dounan, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China, Januari 31, 2023. (Xinhua/Chen Xinbo)

BEIJING - Shirika la Posta la Serikali ya China (SPB) siku ya Alhamisi limeeleza kwamba huduma za usambazaji wa vifurushi nchini China zimeongezeka kwa kasi mwanzoni mwa Mwaka 2023, na kufikia vifurushi bilioni 10 hadi Februari 8.

Kampuni za utoaji huduma za usambazaji wa vifurushi nchini China zilifikia alama ya vifurushi bilioni 10 ndani ya siku 39 za kwanza mwanzoni mwa Mwaka 2023, ambayo ni haraka zaidi kwa siku 40 kuliko Mwaka 2019, kabla ya janga la UVIKO-19 kuanza.

SPB imesema, Ufanisi huu wa mwaka huu unaelezwa kuonyesha uhai, uthabiti na uwezo wa ukuaji wa shughuli za kusambaza vifurushi kwa haraka nchini China, hii inaonyesha kuwa imani ya watumiaji wa huduma hiyo inaongezeka, na kufufuka kwa uchumi kunakua kwa kasi.

Takwimu pia zinaonyesha kuwa wastani wa idadi ya vifurushi vinavyoshughulikiwa kila siku imezidi milioni 330 tangu Mwezi Februari, jambo ambalo limechangia kufufuka kwa soko la watumiaji kwenye ununuzi.

Mwaka huu, SPB itaweka nguvu zaidi kwenye ujenzi wa mfumo wa huduma za usambazaji wa vifurushi vijijini, kuimarisha ushirikiano wa kina wa huduma za posta na viwanda vya teknolojia ya hali ya juu, na kusaidia kujenga makampuni ya kisasa ya kimataifa katika sekta hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha